MANCHESTER UNITED imekubali kumsajili tena kiungo wake wa zamani PAUL POGBA, kutoka kwa mabingwa wa ITALIA ,JUVENTUS
MANCHESTER UNITED imekubali kumsajili tena kiungo wake wa zamani
PAUL POGBA, kutoka kwa mabingwa wa ITALIA ,JUVENTUS na kuvunja rekodi
ya dunia ya pauni milioni100.
Tayari kiungo huyo ameshapita vipimo vya afya alivyofanyiwa siku ya
ALHAMIS usiku jijini LOS ANGELES,MAREKANI. na anatazamiwa kuvaa jezi
namba 6,MANCHESTER inategemea kumtangaza muda wowote kuanzia sasa.
Tangu aondoke united na kujiunga na JUVENTUS mwaka 2012 POGBA kiwango
chake kimepanda na kuwa kiungo mbunifu zaidi duniani kwa sasa.
Je MANCHESTER UNITED inategemea kupata kitu gani kutoka kwa POGBA mwenye umri wa miaka 23?.
Ameifungia JUVENTUS mabao kumi,msimu uliopita,wachezaji wa MAN UNITED
walimpita kwa ufungaji ni ANTHONY MARTIAL aliyefunga mabao 17 na weyne
rooney aliyefunga mabao 15.
Ametoa pasi 12 za magoli kuliko mchezaji yeyote wa SERIA A,huku
mchezaji wa UNITED aliyetoa pasi nyingi za magoli ni ROONEY akiwa
amepiga pasi 6 tu.
Ametegeneza nafasi 54 za mabao,wakati kwa united mchezaji aliyetegeneza nafasi nyingi za magoli ni JUAN MATTA.
Amepiga mashuti,124 na kushika nafasi ya tatu katika SERIA A,ambayo
ni mashuti 54 zaidi ya mshambuliaji wa UNITED ROONEY ambaye ndiye
aliyepiga mashuti mengi zaidi kwa united ,mashuti 70.
Uwezo wake wa kupiga pasi za uhakika ni asilimia 83.4,ambayo haijafikiwa na mchezaji yeyote wa kiungo wa UNITED msimu uliopita.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!