NJIA BORA ZA KUTUNZA VIFAA VYA ELEKTRONIKI NYUMBANI.
Habari za siku na karibu Studio.
Bila shaka haujambo na unaendelea vizuri na michakato ya maisha. Leo
ningependa tuongelee juu ya njia bora za kutunza vifaa vya elektroniki
nyumbani, ofisini na kila sehemu vitumikapo.Njia hizi zitasaidia kwa
namna moja ama nyingine kupata matokeo bora zaidi kutoka katika kifaa
chako husika.
Jinsi ya kutunza Friji na Freezer.
Wengi hutumia kifaa hiki kutunza chakula vivyo hivyo hutumika kupozea
vinywaji baridi. Ili friji au freezer yako idumu zingatia yafuatayo.
- Safisha pembe za mlango wa friji au freezer yako, tumia maji ili kuondoa taka zilizogandamana.
- Punguza barafu iliyoganda katika kuta za friji kwani hizi
husababisha friji kutumia umeme mwingi zaidi na hivyo kukuongezea bili
ya umeme. Unaweza kupunguza au kutoa barafu hizi
kwa kuzima friji hadi ziyeyuke, au futa na maji ya moto, au hair dryer au kwa kutumia feni.
- Usiweke mzigo mzito sana katika shelf za friji au freezer.
- Tumia upepo wa vaccum cleaner ili kupuliza vumbi angalau mara mbili
kwa mwaka, kifaa hiki hupatikana kwa mafundi friji pia mafundi computer.
- Chomoa katika soketi wakati wa mvua.
Jinsi ya kutunza Computer/Laptop
- Update mara kwa mara
- Tumia Antivirus iliyokuwa inayokuwa updated angalau kila siku. Ku
update hakuchukui muda mrefu kama una update kila siku huchukua hata
dakika kadhaa tu. Ninashauri anti-virus hii ya AVG Free Antivirus kwani ni bora sana.
- Zima computer yako kwa kufuata njia mahususi na sio kuchomoa tu nyaya au kuzima ukutani.
- Kwa laptop pindi inapokuwa imetumika kwa muda mrefu na ikachemka
sana jaribu kuizima/sleep/hibernate kwa muda ili ipoe hivyo utasaidia
kuifanya iwe na kasi zaidi.
- Dumisha nguvu na uimara wa betri kama unatumia laptop. Soma post
yangu hii kwa njia zaidi JINSI YA KUBORESHA BETRI LA LAPTOP YAKO LIDUMU
KWA MUDA MREFU.
Tafadhali mpendwa mgeni, je,ungependa kujua zaidi kuhusu kifaa gani na
jinsi ya kukitunza ili kiweze kuwa na manufaa zaidi kwako. Usisite
kinitaarifu nami nitaandaa post kwa ajili yako wewe.
Asante kwa kusoma hii. Nyingine ni bomba pia!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!