Swali: "Ni kwa jinsi gani saikolojia inafanya kazi na ushauri nasaha wa Biblia?"
Jibu:
saikolojia ya kiduniai msingi wake ni kwa mafundisho ya wanasaikolojia
wadadisi kama vile Sigmund Freud, Carl Jung, na Carl Rogers. Kibiblia,
au nautetiki, ushauri nasaha, kwa upande mwingine, msingi wake kimraba
uko katika neon la Mungu lililofunuliwa. Ushauri nasaha wa Biblia
unaona maandiko kama ya kutosha kwa kuandaa mtoto wa Mungu kwa kila
kazi njema (2 Timotheo 3:17). Washauri wa kibiblia hufundisha kwamba
tatizo la kimsingi la mtu ni la kiroho kwa asili; Kwa hiyo,
wanasaikolojia wanaomkana Mungu, ambao ni waliokufa kiroho wenyewe,
hawana ufahamu halisi katika hali ya binadamu.
Katika hali ya kuhusiana, kwa kawaida kinachoitwa"ushauri nasaha wa
Kikristo" ni tofauti na "ushauri nasaha wa Biblia" katika huo ushauri wa
kikiristo mara nyingi unatumia saikolojia ya kidunia kuongezea kwa
Biblia. Hii si kusema kwamba mshauri Mkristo si pia mshauri wa Biblia,
lakini mara nyingi washauri wakristo ni Wakristo ambao huunganisha
saikolojia ya kidunia katika ushauri nasaha wao. Washauri wa Biblia au
nautetiki hukataa saikolojia ya kidunia jumla.
Saikolojia nyingi ni ya kibinadamu kiasili.ubinadamu wa Kidunia hukuza
wanadamu kama kiwango cha juu cha ukweli na maadili na kukataa imani,
isiyo ya dunia, na Biblia. Kwa hivyo, saikolojia ya kidunia ni jaribio
la mtu kuelewa na kukarabati upande wa kiroho wa mtu bila kushauriana na
au utambuzi wa kiroho.
Biblia inatangaza kwamba mwanadamu ni kiumbe cha kipekee cha Mungu,
aliyefanya katika mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26, 2: 7). Biblia waziwazi
inahusika na uroho wa mtu, ikiwa pamoja na kuanguka kwake katika
dhambi, matokeo ya dhambi, na mahusiano ya sasa ya mwanadamu na Mungu.
Saikolojia ya kidunia kwa msingi iko kwa mawazo kwamba mtu kimsingi ni
mzuri na kwamba majibu kwa matatizo yake yako nafsini mwake mwenyewe .
Biblia inajenga picha tofauti sana ya hali ya mtu. Mtu "kimsingi si
mzuri"; yeye ni "mfu katika makosa na dhambi" (Waefeso 2: 1), na moyo
huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye
kuujua." (Yeremia 17: 9). Kwa hivyo, mshauri wa kibiblia kwa haraka
anachukua mbinu tofauti: badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya
kiroho ndani ya akili ya mtu mwenyewe, yeye anatafuta ili kukabiliana na
dhambi, kupata hekima kutoka juu (James 3:17), na kulitumia neon la
Mungu kwa hali hiyo.
Washauri wa kibiblia, kama ilivyo kinyume na wanasaikolojia na baadhi ya
washauri wakristo, wanaangalia Biblia pekee kama chanzo cha mbinu ya
maelezo ya kina kwa ushauri nasaha (2 Timotheo 3: 15-17; 2 Petro 1: 4).
Ushauri nasaha wa kibiblia una msimamo kwa kuruhusu Mungu ajisemee
mwenyewe kupitia kwa neno lake. Ushauri nasaha wa kibiblia unatafuta
kuhudumu upendo wa kweli wa Mungu aliye hai, upendo ambao unashughulikia
dhambi na unazalisha utiifu.
Matibabu ya kisaikolojia ni mahitaji ya msingi. Mahitaji ya
kujithamini, upendo na kukubalika, na umuhimu huelekea kutawala. Kama
mahitaji haya yanaafikiwa , inaaminika, watu watakuwa na furaha, wapole,
na waadilifu; kama mahitaji haya hayajaafikiwa, watu watakuwa wenye
taabu,wenye chuki, na wabaya. Ushauri nasaha wa kibiblia unafundisha
kwamba kuridhika kwa kweli na furaha kunaweza tu kupatikana katika
uhusiano na Mungu na ukimbizaji wa kumcha Mungu. Hakuna kiasi cha
matibabu ya kisaikolojia kinachoweza kumfanya mtu mchoyo asiwe mchoyo,
kwa mfano, lakini mtumishi mtiifu wa Mungu ataridhika katika kutoa kwa
furaha bila uchoyo (2 Wakorintho 9: 7).
Hivyo, jinsi gani saikolojia inafanya kazi na ushauri nasaha wa Biblia?
Kwa kifupi, haufanyi. Saikolojia ya kidunia inaanza na kuishia kwa mtu
na mawazo yake. Ushauri wa kweli wa Biblia unaelekeza wateja kwa Kristo
na Neno la Mungu. Ushauri nasaha wa kibiblia ni shughuli ya
wachungaji,zao la zawadi ya kiroho ya kutia moyo, na lengo lake si
kujithamini balis utakaso.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!