
Mwanafunzi wa kidato cha nne alimteka nyara mtoto wa miaka mitatu baada ya kumpa dawa za kulevya.
Mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya upili ya Maralal kaunti ya
Samburu alisemekana kumteka nyara mtoto wa miaka mitatu baada ya kumpa
madawa ya kulevya.
Mwanafunzi huyo alienda mafichoni na mtoto huyo, huku akimtaka mamake
mtoto kutoa Ksh 170,000 huku akidai kumuua mtoto huyo iwapo hangepewa
pesa hizo.
Joy Lekimain, mamake mtoto alihofia maisha ya mwanawe, jambo lililomfanya kutuma Ksh 2,500.
“Inaonekana alimpa mtoto dawa za kulevya kabla ya kuenda mafichoni
katika kaunti ya Nyahururu,umbali wa kilomita 226 kutoka Maralal.
Alipiga simu akitishia kwamba atamdhuru mtoto iwapo hatapewa fidia ya
Ksh 170,000 kwa muda wa siku tano,” alisema kamanda wa polisi kaunti ya
Samburu,Francis Kumut.
Hata hivyo ilisemekana kuwa mtekaji nyara huyo alikuwa wa jamii moja na mtoto huyo .
Alipatikana siku sita baadae akiwa amejificha kwenye nyumba moja katika mtaa wa Chang’aa kaunti ya Nyahururu.\
COMMENT AND SHARE........................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!