
Kuna habari imesambaa mtandaoni kuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi hiyo Augustine Chihuri
kuwakamata wachezaji wote wa timu iliyokwenda kushiriki michuano ya
Olimpiki nchini Brazil.
Inasema Mugabe amechukua hatua hiyo baada ya kuumizwa na wachezaji hao
kushindwa kupata hata medali moja kwenye mashindano hayo huku pesa
iliyowekezwa kwenye timu ili kuiwakilisha nchi ingeweza kutumiwa
kununulia dawa na kujenga shule.
“Jambo hili ni sawa na mwanaume asiyelijali kuoa wanawake watano, maana
yake nini? Nitahakikisha tunagawana hasara, wote watailipa serikali bila
kujali huku wakijua kuwa fedha zilizowapeleka huko zinatoka kwenye
mifuko ya wananchi,” Mugabe anadaiwa kusema.
“Tumepoteza pesa za taifa kwa ajili ya hao panya tunaowaita wanamichezo.
Kama hauko tayari kujitoa na kushinda japo medali ya shaba kama wenzetu
wa Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda kupoteza pesa zetu,”
ameongeza.
Cha kuchekesha zaidi, Mugabe alidaiwa kusema, “kama tulihitaji watu
kwenda Brazil kuimba wimbo wetu wa taifa na kupeperusha bendera,
tungewaagiza warembo na vijana watanashati kutoka Chuo Kikuu cha
Zimbabwe wakatuwakilishe.”
Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ambayo wanamichezo wake hawakufanikiwa
kushinda medali ikiwa inawakilishwa na wanamichezo 31. Mchezaji ambaye
alionekana kufanya vizuri ni yule aliyekamata nafasi ya nane.
Hata hivyo kuna uwezekano habari hii inaweza kuwa ni ya kutengenezwa
(satire) kama nukuu mbalimbali za kuchekesha ambazo amekuwa akidaiwa
kuzisema.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!