
Mwezi huu umekuwa wa mapambano makubwa kati ya vituo vya redio viwili jijini Dar es Salaam, Clouds FM na EFM.
EFM walibomoa kipindi cha Power Breakfast kwa kuwachukua Gerald Hando,
Paul James na mtayarishaji wa kipindi hicho, Abel Onesmo huku Clouds FM
wakikibomoa kipindi cha Ubaoni cha EFM kwa kumchukua mtangazaji wake wa
zamani, Gardener G Habash.
Gardener aka Captain anaanza kazi rasmi Jumatatu hii kwenye msimu mpya
wa kituo hicho kwa kuendelea kukiendesha kipindi chake cha zamani,
Jahazi.
Mtangazaji huyo anadaiwa kupewa mshahara mnono unaoweza kumfanya kuwa
mtangazaji anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko wote Tanzania. Kwanza
miongoni mwa vitu alivyopewa ili kurejea tena CMG ni gari aina ya Land
Rover Discovery na mashavu mengine mengi.
Kwa upande wa EFM kuna kila dalili kuwa kipindi chao cha asubuhi
kitapata nguvu mpya kuanzia wiki hii. Haijulikani ni watu wapi Clouds FM
wamewachukua kuziba pengo lililoachwa kwenye Power Breakfast.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!