Mwanamke mmoja aliyezaliwa Somalia lakini sasa ni mpiganiaji haki za
kibinadamu Ilhan Omar anapigiwa upatu kuweka historia kuwa Mmarekani wa
kwanza mzaliwa wa taifa hilo la Afrika Mashariki kuchaguliwa kuwa mbunge
nchini Marekani.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 33 amemuangusha
mbunge aliyehudumu kwa zaidi ya mika 44 katika bunge la jimbo la kwa
chama cha Democratic .
Mbunge huyo wa zamani bi Phyllis Kahn amekuwa akiiwakilisha DFL, kinachoshirikiana na chama cha Democratic .
Bi
Omar, na familia yake walitoroka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini
Somalia kwenda Kenya walikoishi kwa miaka minne kabla ya kwenda
Marekani.
Huko walihamia eneo lenye wasomali wengi la Cedar-Riverside, katika jimbo la Minnesota.
Kizingiti
kilichosalia mbele ya bi Omar ni mpinzani wake wa chama cha Republican
Abdimalik Askar, ambaye pia ni msomali raia wa Marekani katika uchaguzi
mkuu ujao ulioratibiwa kufanyika mwezi Novemba.
Hiyo inamaanisha iwapo kila hali itasalia ilivyo basi Msomali mmoja raia wa Marekani atakuwa bungeni mwakani.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!