Mo Dewji Aanza Na Mishahara Simba SC:;
MFANYABIASHARA anayetaka kununua hisa ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed
Dewji ‘Mo’, ameanza kasi ya kuitumikia klabu hiyo ya Simba kwa kuanza
kulipa mishahara ya wachezaji kuanzia mwezi huu huku suala la kununua
hisa likitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.
Hatua hiyo ya Mo imekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kuridhia
kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wa sasa wa wanachama na
kwenda kwenye mfumo wa hisa, kufuatia Mo kuhitaji kununua hisa asilimia
51.
Mohamed Dewji ‘Mo’ (kushoto) akisalimiana na viongozi wa Simba.
Aidha, kamati itaandaa mkataba wa maridhiano ili kila upande uweze
kutekeleza majukumu yake ambapo Mo alieleza kuwa ataisaidia timu hiyo
huku akiwa anaendelea kusubiria mchakato wa hisa kukamilika.
Akizungumza na Championi Jumamosi, mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji
Simba ambaye aliomba jina lake lifichwe, alisema Mo ataanza kuwalipa
wachezaji mishahara kuanzia mwezi huu.
“Kwa sasa kuna kamati imepewa kazi ya kuwaelimisha wanachama juu ya
suala hilo ili kuweza kufahamu faida gani watakayoipata juu ya suala
hilo ili mwisho wa siku yafanyike maamuzi sahihi.
“Kwa kuanza, ataanza na kuwalipa mishahara wachezaji ambapo itaanzia
mwezi huu na atapewa majina ya wachezaji wanaotakiwa kulipwa mishahara
ili aweze kuwalipa wachezaji wote lakini jukumu alilopewa ni juu ya timu
tu kwa sasa lakini mambo mengine yote yatabaki chini ya uongozi.
“Suala lake nadhani litachukua muda mrefu hata mwaka mmoja hadi kufikia
kukamilika kwa mchakato mzima kufuatia kupata maoni mbalimbali na
makubaliano kutoka kwa wanachama baada ya kupata elimu ya kutosha.
“Hata hivyo asilimia kubwa ya wanachama hawataki auziwe hisa kubwa ya
asilimia 51 na badala yake auziwe asilimia 48,” alisema bosi huyo.
Alipotafutwa Msemaji wa Simba, Haji Manara kuzungumzia suala hilo, simu
yake iliita bila ya kupokelewa hata katibu, Patrick Kahemele naye simu
yake haikupokelewa.
Tayari Mo alishatoa msaada wa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia
usajili, kiasi ambacho Simba ilikitumia kwa ajili ya kukamilisha
usajili wa wachezaji kadhaa nyota walionao hivi sasa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!