Raia mmoja wa MAREKANI amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwadhalilisha kijinsia watoto
Raia mmoja wa MAREKANI amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela baada ya
kupatikana na hatia ya kuwadhalilisha kijinsia watoto wanane yatima
wanaotunzwa kwenye kituo cha watoto yatima nchini MALAWI.
Gazeti la Nyasa Times limesema GERALD CAMPBELL, amekiri katika
mahakama ya TEXAS , MAREKANI kujihusisha na vitendo hivyo vya
udhalilishaji kwa watoto hao wadogo wakati wakiwa chini ya uangalizi
wake katika kituo hicho kati ya mwaka 1997 na 2009.
Kwa mujibu wa CAMPBELL, aliwaruhusu watoto kuingia nyumbani kwake
kutumia maji ya moto na vifaa vingine, kisha kuwafanyia udhalilishaji
huo.
CAMPBELL baada ya kumaliza kifungo chake atakuwa chini ya uangalizi
kwa kipindi chote cha maisha yake ambapo pia atatakiwa kulipa fidia ya
dola Elfu-40 za kimarekani kwa kosa alilolifanya
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!