Mitaji imekuwa kikwazo kikubwa katika kuanza biashara nyingi sana. Sababu nyingine ni kuwa watu wengi wanaofikiria kuanza biashara
wanataka kuanza na mitaji mikubwa kama milioni 5 -10 au zaidi. Ukweli
ni kwamba hiyo ni ngumu hasa kwa nchi ambazo ni maskini kama Tanzania.
Mwishowe mawazo mengi ya biashara yanakufa kabla ya kuanza.
Wataalamu wa bishara wanaeleza kuwa kuanza ni kugumu na ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya wajasiliamali wengi
Ukweli ni kuwa kuna biashara nyingi tu ambazo hazihitaji mitaji mikubwa kuanza.
1. Kufundisha

Tafuta kitu ambacho unakifahamu na angalia jinsi utawapa watu elimu yako.
Mfano unaweza ukawa ni mtaalamu wa kupika keki tamu. Basi unaweza
ukaanda darasa la watu katika maeneo unayoishi na kuandaa mafunzo kwa
ada ndogo nyumbani kwako.
Unahitaji kiasi kidogo tu cha fedha ili kutimiza hilo.
Pia unaweza ukafundisha watoto masomo ya ziada kama hesabu au sayansi kama unaufahamu wa masomo hayo au mengineyo.
Vyote hivi havihitaji hela nyingi kuanza kwasababu huhitaji chumba cha biashara wala fanicha.
2. Biashara ya Mtandao

Jiunge na kampuni inayofanya masoko kwa njia ya mtandao. Makampuni
haya yatakuhitaji wewe kuafanya matangazo kwa njia ya mdomo kwa mtu hadi
mtu kwa kuwaeleza juu ya bidhaa za kampuni husika na wakinunua basi
kampuni itakulipa wewe kiasi cha fedha kwa mauzo yaliyofanyika.
Usajili katika biashara hii kunahitaji mtaji mdogo sana hata kwa Sh. 100,000 tu unaweza ukaanza na kuendelea kukuza mtaji.
Baadhi ya biashara za mtandao kuanza
3. Kutoa Ushauri wa Kitaalamu

Kama wewe ni mtaalamu katika nyanja fulani kama vile fedha,afya au
komputa kwa mfano,unaweza ukaanzisha huduma ya ushauri kwa makampuni
madogo au watu binafsi.
Ili kufanya hivyo utahitaji fedha kidogo tu kwaajili ya vitendea kazi kama vile karatasi, kalamu n.k
Utahitaji kujitangaza kwa kupita ofisi hadi ofisi au kwa kutoa matangzao katika radio ,TV au magazeti.
Unaweza kutumia ofisi za wateja kwajili ya kazi hii hivyo kuwa na
ofisi. Tumia sehemu unayoishi kama ofisi hivyo ngarama itakuwa ndogo
sana.
4. Huduma ya Kutunza Watoto Wadogo

Kutunza watoto wadogo kati ya mwaka 1-5 ni biashara ambayo unaweza
ukaianzisha na kuifanya nyumbani na itahitaji fedha kidogo tu.
Wazazi wenye watoto wanahitaji sehemu ambayo watoto wao watapata huduma wao wakiwa kazini.
Kama ukianda mazingira mazuri ampapo watoto wanaweza kucheza na kujifunza,basi utapata wateja wengi.
5. Kukodisha Hema

Huduma ya kukodisha hema kwaajili ya shughuli ni mijawapo ya biashara ambazo hazihitaji mitaji mikubwa.
Utahitaji hema moja au mawili ili kuanza na kisha unaweza ukaongeza kadiri unavyoendelea na kukua.
Uhitaji wa hudum hii ni mkubwa hasa katika shrehe za harusi,siku za
kuzaliwa,kipaimara ,komunio,maulidi na bia katika shughuli za misiba.
Mwisho
Biashara zote nilizozitaja hazihitaji fedha nyingi kuanza,kiukweli Shilingi 100,000 tu au pungufu zinatosha.
Hivyo kama unafikiria kuanza bishara na huna mtaji wa kutosha;basi fikiria mojawapo kati ya hizi na ufanikiwe.
Ningependa kusikia biashara nyingine kama hizi. Andika katika kisanduku cha maoni hapa chini nautume.
COMMENT AND SHARE........................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!