Shilingi Milioni 48 zimechangwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya
chekechea ya kisasa na uzio wa kanisa katoliki Parokia ya watakatifu
PETRO na PAULO
Shilingi Milioni 48 zimechangwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya
chekechea ya kisasa na uzio wa kanisa katoliki Parokia ya watakatifu
PETRO na PAULO Mitume SHANGANI Magharibi manispaa ya MTWARA, MIKINDANI.
Fedha hizo na vifaa mbalimbali vya ujenzi zimechangwa wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule mjini MTWARA.
Akizungumza katika harambee hiyo Mkuu wa mkoa huo HALIMA DENDEGO
amewataka wazazi na walezi kuwapeleka shuleni watoto waliofikisha umri
wa kuanza shule.
Mapema mwenyekiti wa parokia hiyo OPORTUNA KOMBA na Kaimu Askofu wa
jimbo la MTWARA Padri PATRIC MWAYA wamesema shule hiyo inalenga
kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye ulemavu.
Ujenzi wa shule hiyo ya chekechea ya kisasa pamoja na uzio wa kanisa utagharimu Shilingi Milioni 600 .
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!