Mfalme wa JAPAN AKIHITO ameeleza mpango wake wa kutaka kung'atuka kutokana na umri mkubwa aliokua nao
AKIHITO mwenye miaka 82 amesema ana wasiwasi kuwa huenda ikawa vigumu
kwake kutekeleza majukumu yake kutokana na kuzorota kwa afya yake.
Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema kulikua na vipingamizi
katika mpango wa kupunguza majukumu ya mfalme kama nembo ya taifa.
Watu wengi wamekua na mitazamo tofauti kuhusu taarifa hiyo lakini
hata hivyo hatua hiyo inahitaji mabadiliko ya sheria ya JAPAN ambapo kwa
sasa hakuna nafasi kisheria inayomruhusu mfalme kuondoka madarakani.
Waziri Mkuu wa JAPAN, SHINZO ABE, amesema atatathmini kwa makini matamanio ya mfalme huyo.
Akizungumza muda mfupi baada ya hotuba ya Mfalme AKIHITO Waziri Mkuu
amesema atazingatia nini kinachoweza kufanywa na serikali kwa ajili ya
Mfalme. Mfalme AKIHITO amekuwa madarakani tangu mwaka 1989 baada ya kifo
cha baba yake, HIROHITO.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!