atika ulimwengu wa
mapenzi, kila siku watu wanaingia kwenye uhusiano lakini elewa kwamba
siku ambayo wewe unamzimikia mtu flani siku hiyo hiyo wapo
wanaozinguana na kuachana.Si
kwa wapenzi tu, hata kwenye ndoa wapo ambao leo hii ndiyo wanaoana
lakini leo hii hii kuna wanaopeana talaka. Iko hivyo na kwa maana hiyo
suala la kupendana lipo lakini la kuachana nalo halikwepeki.Ndiyo
maana ukijaribu kufuatilia hata wewe unayesoma makala haya yawezekana
mpaka umefikia hatua uliyonayo umeshaacha au kuachwa. Hilo
ndilo limenifanya niandike mada hii. Je, unajua mbinu sahihi za
kumuacha mtu ambaye mlikuwa mkiambiana I love you, I love you too? Kama
jibu ni hapana, leo nitakupa shule inayoweza kukuongoza katika hilo.
Lakini
kabla ya kulizungumzia hilo niseme tu kwamba miongoni mwa vitu
nisivyovipenda katika maisha yangu ni kusikia flani na flani waliokuwa
wanapendana sana hadi kuwa gumzo mtaani wameachana.
Inaniuma kwa
sababu najua ivavyouma. Mara nyingi anayeachwa anaumia zaidi hasa akiwa
hajajiandaa na ndiyo maana wataalamu wa masuala ya mapenzi wamejaribu
kuanisha mbinu ambazo unaweza kuzitumia katika zoezi zima la kumuacha
mpenzi au mume/mke wako hasa pale zinapokuwepo sababu za msingi
zinazoweza kukubalika.
1. Hakikisha umedhamiriaUnatakiwa
uwe umejiandaa kumkosa katika maisha yako. Jadiliana na akili pamoja
na moyo wako kama kweli vimeridhika na uamuzi unaotaka kuchukua.
Jiulize ni kweli amekukosea kiasi kwamba huwezi kuendelea kuwa naye?
2. Usiwe mwenye hasira
Unapotaka
kumuacha mpenzi, mume au mke wako kwa sababu maalum, hakikisha huna
hasira.Tulia ili hata pale utakapokuwa hauko naye usije ukajuta na
kudhani hukuchukua uamuzi sahihi.
3. Muda na siku sahihiWataalamu
wa mapenzi wanasema kuwa, muda wa asubuhi siyo mzuri kumuacha mpenzi
wako kwani utampa wakati mgumu siku nzima lakini pia kwa wapenzi
wanaofanya kazi siku za katikati ya wiki siyo siku nzuri.
Siku ya
Ijumaa jioni inapendekezwa kuwa siku nzuri ya kumuacha mpenzi wako kwa
maelezo kwamba ataitumia wikiendi kujiliwaza na hata inapofika Jumatatu,
anakuwa amepoa tayari kwa kuendelea na majukumu yake.
Kama
nilivyosema awali, kila siku watu wanaingia kwenye uhusiano mpya lakini
pia wengine wanaachana. Sababu za kuachana kwa wapenzi zinatofautiana
ila kikubwa ni kwamba unapoachana na mtu ambaye mlikuwa ‘mwili mmoja’
hutakiwi kumgeuza adui yako kwa asilimia zote, hata kama kakukosea
vipi.
Kwa mfano, yawezekana ulitokea kumpenda na kuhisi angeweza
kuwa wako wa maisha lakini kadiri siku zinavyokwenda unabaini si mtu
sahihi kwako. Katika mazingira hayo suala la kumuacha haliepukiki ila
cha kujiuliza ni kwamba utamuachaje?
Je, itakuwa ni sahihi
kumuambia laivu kwamba mimi na wewe basi? Inawezekana ukafanya hivyo
ila wataalam wa mapenzi hawashauri kwani wanajua madhara ya kutumia
mbinu kama hiyo na ndiyo maana wakashauri kutumia njia ambazo zinaweza
kusaidia ukamuacha lakini bila kumuumiza na maisha yakaendelea kuwepo.
Jitoe taratibuChukulia
kwamba umekuwa naye kwa muda mrefu kidogo ukiwa na malengo ya kuingia
naye kwenye ndoa lakini katika utafiti wako ukabaini hakufai,
unashauriwa kujitoa kwake kimyakimya. Unachotakiwa katika mbinu hii ni
kupunguza kumtendea mambo ya kiupendo.
Kwa mfano, unaweza kupunguza
kuonana naye, kumpigia simu, kumtumia sms na hata kumsaidia kifedha
kama ulikuwa ukifanya hivyo. Kwa kufanya hayo ni lazima ataanza kuona
tofauti na kuhisi penzi linaelekea ukingoni.
Aidha, kwa kumfanyia
hivyo ni lazima atahoji juu ya mabadiliko hayo. Wewe hutakiwi kutoa
maelezo yoyote zaidi ya kuendelea kuyeyusha bila kumwambia wazi kwamba
umemtoa moyoni mwako.
Kama huyo mpenzi wako ni mwelewa atagundua
kuwa, ndiyo unamuacha kimtindo na yeye ataanza kujiandaa kukukosa, hata
pale utakapokata mawasiliano moja kwa moja atakuwa ameshajua kuwa
umemuacha hata bila kumueleza.
Ukigundua ameshafahamu kuwa
umemuacha, hapo unaweza kumwambia kwa kifupi kwamba umeamua bora kila
mmoja aendelee na maisha yake. Kisaikolojia utakuwa hujamuumiza sana
lakini tayari utakuwa umemuacha.
Maneno ya busaraUnaweza
kumuacha mpenzi wako kwa kutumia lugha ambayo yeye mwenyewe atahisi
hukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima umuache. Mfano: ‘Ashura, kusema
ukweli nilikupenda sana na mpaka sasa naamini wewe ni mwanamke wa maisha
yangu, sikuamini kama yupo mwanamke mwingine wa kunipa furaha kama
wewe lakini kwa hili lililotokea sina jinsi, inabidi nikuache.
Utaendelea kuwa rafiki yangu na kama ni kukusaidia nitakusaidia kama
rafiki na si mpenzi.”
Hayo ni maneno ambayo mwanaume anamwambia
mpenzi wake akimaanisha anamuacha lakini ukiyachunguza utabaini
hayachomi sana kwa kuwa anayeachwa bado anapewa nafasi nyingine ya
urafiki wa karibu na si mapenzi tena.
Mimi nikushauri tu kwamba,
hakikisha unapotaka kuachana na mtu ambaye mmekuwa pamoja kwa muda
mrefu unakuwa makini. Hata kama amekukosea vipi lakini busara itumike
hasa kwa kuzingatia yale mazuri ambayo aliwahi kukufanyia huko nyuma.
:;
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!