Marekani yawawekea vikwazo wanaye Joseph Kony:;
Marekani imesema kuwa imeweka
vikwazo vya kiuchumi dhidi ya watoto wawili wa kiume wa kiongozi wa
kundi la Lord's Resistance Army (LRA) leader Joseph, ikiwashutumu
kuhusika katika biashara haramu ya kusafirisha pembe za ndovu.
Salim
Kony na Ali Cony walikua makamanda wa LRA waliokuwa na '' nafasi
kubwa " katika biashara ya usafirishaji wa pembe za ndovu kutoka mbuga
ya wanyama ya Garamba iliyopo kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo kupitia taifa jirani la Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) hadi
katika jimbo linalozozaniwa la Kafia Kingi kwa ajili ya mauzo ama
biashara na wanunuzi wa jimbo hilo, ilieleza kauli ya mamlaka ya hazina
ya Marekani.
Huku Salim akiratibu shughuli za usafiri wa pembe
za ndovu, Ali amekua muhusika mkuu katika kujadili na wafanya biashara
viwango vya bei na huuza pembe hizo kwa dola ama pauni ya Sudan, ame kwa
mauzo ya ya pembe za ndovu kwa silaha , makombora, na chakula na
wachuuzi wa Kafia Kingi."
Mali yoyote inayomilikiwa na wanaume hao
wawili nchin Marekani nchini Marekani itafujwa na "kwa ujumla" raia
wa Marekani wanazuiwa kufanya biashara nao, alisema mkuu wa hazina .
Kundi la LRA liliundwa nchini Uganda, lakini lilifurushwa nchini humo na vikosi vya serikali.
Wapiganaji wake sasa wamekua wa kuhama hama katika maeneo ya misitu mikubwa ya DRC na Jamuhuri ya Afrika ya kati.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!