Manukato yaweza kusaidia kukabiliana na uhalifu, wanasema watafiti
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Manukato yaweza kusaidia kukabiliana na uhalifu, wanasema watafiti:;
Wanasayansi wamebaini kuwa kemikali
zinazotengeneza manukato zinaweza kuhama kutoka kwenye nguo ya mtu mmoja
hadi mwingine, hata kama wamegusana kidogo.
Harufu ya manukato inaweza kubaki kwenye nguo kwa siku kadhaa , licha ya kwamba huisha baada ya muda.
Jopo
la wanasayansi hao linasema huu ni ushahidi wa msingi wa utafiti,
lakini wanasema kwamba manukato yana uwezekano mkubwa wa kutumiwa kupata
ushahidi wa uhalifu.
Katika taarifa yao waliyoindika katika
jarida la kisayansi na haki,watafiti hao wanasema walifanyia uchambuzi
harufu za manukato zinazoweza kufaa katika visa ambako kumekuwa na
mgusano wa karibu wa kimwili kama vile kesi za uhalifu wa kingono.
Katika taarifa yao waliyoindika katika jarida la
kisayansi na haki,watafiti hao wanasema walifanyia uchambuzi harufu za
manukato zinazoweza kufaa katika visa ambako kumekuwa na mgusano wa
karibu wa kimwili kama vile kesi za uhalifu wa kingono.
Mkuu wa utafiti huo Simona Gherghel, kutoka University
College London, anasema : " Tulihisi kuna uwezekano mkubwa wa kutumiwa
kwa manukato kwasababu wahu wengi ni watumiaji''.
''Tunafahamu asilimia 90% ya wanawake na asilimia 60% ya wanaume wanaotumia manukato kila siku'',
''
Wakati tunafahamu kuwa kazi kubwa katika katika sayansi ya kutafuta
ushahidi ulio hamishwa - hadi sasa haujawahi kufanyika utafiti kuhusu
kuhamishwa kwa manukato kutoka mtu mmoja kuelekea mwingine ."
Manukato ni mchanganyiko wa kemikali mbali mbali, ambazo zikichanganywa humpatia mtu binafsi harufu ya kipekee aipendayo .
Watafiti
walipochunguza aina moja ya manukato ya wanaume , walibaini kuwa
mchanganyiko huu wa kemikali uliweza kuhama kutoka kipande kimoja cha
nguo iliyotengenezwa kwa pamba hadi kipande kingine cha nguo ya pamba.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!