Muanzilishi na mfalme wa nyimbo za singeli Msaga Sumu kama mwenyewe
anavyojiita amesema yeye hajali bifu ambazo wasanii wenzake wa visingeli
wanazomuundia
Akizungumza
ndani ya eNewz amesema “ huwezi ukaamini bifu na mimi wameanza tangu
naanza ni kweli wanakuja na wapo wengi hao watoto lakini naweza
kuwaambia bifu na mimi wanashindwa kwa sababu mimi ni mtu ambaye
naangalia maisha kuliko bifu.
Mimi ninachokumbuka nilimuambia kama anataka muziki uwe wa maisha
yako jifunze kukomaana mi naona ameamua kuzingatia kwa kuwa naona wimbo
wake huu wa 'hainaga ushemeji' kidogo umepita japo haujazidi wimbo wangu
wa “Shemeji unanitega” aliendelea kusisitiza Msaga Sumu.
Msaga sumu alimalizia kwa kusema “naweza kusema ndo maana wananiwekaa
juu kwa maana kila ninapotoa mimi na wao wa wanafata hicho hicho yaani
hawana ubunifu ninachotaka kuwaambia kama wanataka kuja ili mziki wa
kisingeli ufike mbali wajitahidi kubuni na si kusubiri Msaga Sumu abuni
alafu waige.
Hata hivyo kwa upande wa Man Fongo aliisema “Mimi naangalia alama za
nyakati naangalia mziki unaelekea wapi na mimi sitaki ufalme wala nini
na kama wapo walioanza sitaangalia walianzia na ladha mimi naimba
singeli hivyo sitaangalia anachokifanya mtu yeyote.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!