Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Lowasa na Magufuli Wakutana Live Uso kwa uso Jubilee ya Ndoa ya Mkapa

           Hafla ya Jubilei hiyo imefanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay na imetanguliwa na Misa ya shukrani iliyofanyika katika kanisa hilo majira ya asubuhi.

Jubilei hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Mhe. Edward Lowassa.

Misa Takatifu ya Shukrani imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa na Maaskofu na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa na ameeleza kuwa ndoa hiyo iliyowaunganisha wanandoa wanaotoka katika madhehebu tofauti ya Kikristo imetoa fundisho kubwa kuwa binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama wana tofauti mbalimbali zikiwemo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda.

Rais Magufuli amesema miaka 50 ya ndoa ya Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa ya Shukrani na Jubilei hiyo ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.

Rais Mstaafu Mkapa pia ametoa wito kwa watanzania kupenda na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa "Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake"
Naye Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.

Kardinali Pengo amesema ndoa ya Rais Mstaafu Mkapa anaifundisha jamii kuwa tunaweza kuishi kwa imani zetu bila kubadili dini.




COMMENT AND SHARE..........
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube