Lowasa Apigilia Msumari Operesheni UKUTA, Asema Haiwezekani Mtu Mmoja Azuie Kila Kitu:;

Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,
UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo ,
tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya
nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .
CHADEMA ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu
,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi
nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya
mtu fulani .
Najua polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila
niwahakikishie wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya
Kimataifa .
Siasa ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya
mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September
Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu
wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe
kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na
majimbo nchi nzima .
Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.
Kamati kuu ilipoamua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu
yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye
busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki
ya watanzania wote.
Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama
wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na
kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma "- LOWASSA
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!