MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na Mwarabu mmoja ambaye
jina lake halikuweza kupatikana mara moja, wamezua utata wa aina yake
kufuatia msanii huyo ‘kumposti’ mara kwa mara kwenye mtandao wake wa
Instagram.
Risasi Jumamosi lilianza kumfuatilia Jide baada ya kutonywa na chanzo
kuwa msanii huyo amekuwa akimposti Mwarabu huyo na kwamba kuna kila
dalili ni mtu wake aliyerithi mikoba ya aliyekuwa mumewe, Gardner
Habash.
JIDE“Nyie kama vipi fuatilieni kwa makini kwenye Instagram yake,
mtagundua tu ukweli, kuna kitu maana hata akimposti huyo jamaa huwa
anaweka maneno yenye utata, hataki kufunguka moja kwa moja kama ni
mpenzi wake au vipi,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kulitonya Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu
aliingia kwenye ukurasa wa Jide na kuziona picha tofauti zikimuonesha
akiwa amekaa na Mwarabu huyo huku akisindikiza na ujumbe ambao hautoi
majibu ya moja kwa moja kama ni mtu wake au la.
JideAlipotafutwa mrembo huyo kupitia simu yake ya mkononi, iliita
bila kupokelewa lakini mmoja wa mameneja wake alisema mwanaume huyo ni
rafiki wa karibu wa Jide na kama kutakuwa na lolote, atafafanua baadaye.
“Ni rafiki yake tu na nisingependa kumtaja jina lake maana sidhani
kama ni jambo zuri, nyie msiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa wazi tu
muda muafaka utakapowadia, najua watu wengi mnataka kumjua shemeji mpya,
wawe wavumilivu tu watamjua,” alisema meneja huyo huku akiomba hifadhi
ya jina.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!