KWA NINI UPWEKE NI HATARI KWA AFYA?:;
Kuwa mpweke kwaweza kuwa hatari kwa afya mara mbili zaidi
ya hatari itakanayo na kuwa na uzito mkubwa, kutokana na utafiti uliofanyika,
mtu anapohisi kutengwa, au kutengwa na jamii yake inakuwa hatari sana husani
mtu huyo anapokuwa amefikisha umri wa kati.
Utafiti uliofanyiwa kwa watu walio na umri zaidi ya
miaka 50 umegundua kuwa watu waliokuwa wapweke walikuwa katika hatari ya kufa
mapema mara mbili zaidi ya wale waliokuwa wamezungukwa na jamii zao,
matokeo
hayo yalionekana baada ya miaka mingi ya utafiti huo.
Katika utafiti huo, ulinganisho wa wastani wa idadi ya
watu waliofanyiwa utafiti, wale waliosema walikuwa wapweke walikuwa na asilimia
14 ya hatari ya kufa mapema. Kiwango hicho ni mara mbili ya hatari itokanayo na
kuwa na uzito mkubwa kati ya hao waliofanyiwa utafiti.
Utafiti uliofanyika kwa wale walio wazee huko
Uingereza katika mwaka wa 2012 wanasayansi waligundua kuwa, wazee wengi walijihisi wapweke
na waliotengwa muda wote, na hali hiyo ya kutengwa iliongezeka zaidi wakati wa
mwisho wa wiki(weekend) na nyakati za usiku.
Tafiti nyingi zilizofanyika zimeonyesha kuwa, upweke
unahusiana moja kwa moja na magonjwa kama
shinikizo la damu, udhaifu wa kinga ya mwili, hatari kubwa ya kupata msongo wa
mawazo, shambulizi la moyo na kiharusi.
“Watu huwa na mtazamo usio wa kawaida kuhusu kustaafu kazi.
Wengi hufikiri kustaafu ni kutengana na
marafiki, familia na watu wengine na kutafuta sehemu tulivu za kumalizia maisha
kwa furaha. Lakini inawezekana hilo sio jambo zuri “ mwandishi wa kitabu cha upweke (Loneliness) John
Cacioppo alisema.
Watu ambao wataendelea kuwa karibu na wafanyakazi
wenzao,familia zao, marafiki na ndugu wengine baada ya kustaafu wanazidi kuwa
wachangamfu na wasio na upweke. Kuwa na muda wa kufurahia maisha na tumia
nyakati za furaha na familia na marafiki. Watu wasio wapweke ni wale walio
karibu na familia, marafiki na jamaa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!