Habari hii imeripotiwa na BBC Swahili kuhusu jamii moja nchini Malawi ambayo haithamini ubikira wa watoto
wao wa kike. BBC Swahili wameripoti kuwa katika jamii hiyo wazazi
wanamlipa mwanaume kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya
kwanza.
Jamii hiyo inaamini kwamba kuwa na binti ambaye ni bikira
ni mkosi kwa jamii, wazazi na jamii kwa ujumla katika maeneo mengi ya
kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na miaka.
Wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi,
na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha
kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa ‘fisi’.
Mafisi hulipwa takriban dola 7 ambayo ni kama Tsh 15,324 kwa kila
kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa
miaka 11-14. Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia
BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi……
”kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya
wasichana 104, hiyo ndio tamaduni zetu pia hapa mwanamke akifiwa lazima
aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe’‘.
COMMENT AND SHARE.....................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!