KUPANGA UZAZI KWA KUTUMIA NJIA YA KALENDA:;
Njia ya kutumia kalenda ya uzazi wa mpango ni mojawapo ya
njia ambazo hukadiria ni wakati gani mwanamama huweza kupata ujauzito, na
misingi yake ni uelewa na kuweka rekodi ya mizunguko ya hedhi ya miezi
iliyopita.
Mwanamama anaweza kutumia Njia ya wanaopata siku za
hedhi za kawaida kama siku zake za mzunguko wa hedhi ni kati ya siku 26 hadi 32
kwa urefu.
Kama mwanamama atakuwa na mizunguko ya hedhi zaidi ya 2 ndani ya mwaka
ambayo ni mirefu au mifupi ukilinganisha na mizunguko ya kawaida ya hedhi, njia
hii ya kawaida ya kalenda haitaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Kalenda, kalamu, simu ya mkononi (ukipenda)
Fuatilia na weka
rekodi ya siku za mizunguko ya hedhi.
|
- Mwanamama
afuatilie siku za mzunguko wake wa hedhi, akihesabu siku ya 1 pale anapoona
siku zake.
|
Epuka tendo la ndoa
bila kinga kati ya siku ya 8 hadi siku ya 19.
|
- Siku
ya 8 hadi ya 19 ya mzunguko hedhi, mwanamama mwenye mzunguko wa kawaida
anaweza kupata mimba.
- Wapenzi
waepuke tendo la ndoa bila kutumia kinga.Waweza kutumia kinga kama kondomu
kuanzia siku ya 8 hadi 19.
- Wapenzi
wanaweza kufanya tendo la ndoa bila kinga siku ya 1 hadi ya 7, tangu
mwanamama aanze kuona siku zake, pia anaweza kushiriki tendo la ndoa bila kinga kuanzia siku ya 20 hadi atakapoona
siku zake za mzunguko unaofuata.
|
Tumia viweka
kumbukumbu
|
- Mwanamama
anaweza kutumia kalenda kwa kuweka alama ili kuepuka kusahau. Katika zama
hizi za sayansi na teknolojia pia simu yako ya mkononi yaweza kutumika kwa
kutega milio ambayo itakukumbusha siku maalum.
|
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!