Kocha mpya wa timu ya TAITFA ya ARGENTINA, Edgardo Bauza amesema anataka
kumshawishi nahodha wa zamani wa timu hiyo Lionel Messi akubali
kubadili mawazo yake na kurejea kuchezea tena timu hiyo.
MESSI alichukua uamuzi wa kustafu kuichezea timu hiyo mwezi
JUNE mwaka huu baada ya kukosa mkwaju wa penati na kupoteza kwa mara ya
tatu mchezo wa fainali dhidi ya CHILE kwenye michuano ya COPA AMERICA.
BAUZA alichukua nafasi ya Gerardo Martino aliejiuzuri amesema malengo
yake kwa sasa ni kutaka kuongea mambo ya soka na MESSI hivyo njia hiyo
itasaidia kumshawishi kurejea kuichezea timu ya TAIFA.
Kocha huyo ameongeza kwa kusema pili atamueleza mipango yake na
atamsikiliza MESSI anataka nini na hapo atamueleza umuhimu wake kwenye
timu ya TAIFA hivyo anahakika atakubali ombi lake.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!