Kitunguu Swaumu hutibu magonjwa 30:;
Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi
maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu
katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya
na ustawi wetu. Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa
na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni
kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa
Allium sativum.
Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani
Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu
nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu
mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi
mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo
katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China
mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha
wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani
Afrika walivitumia sana.
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur
aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali
vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya
kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza
na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa
kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo
(mouth wash).
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika
kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi
kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea
kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani
hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora
wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na
ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka
katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una
friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo
nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au
mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila
unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya
kila siku.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja

kitunguu swaumu
Kigawanyishe katika punje punje

kitunguu swaumu
Menya nusu yake (punje 8 au 10 hivi),

kitunguu swaumu
Menya punje moja baada ya nyingine

kitunguu swaumu
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu

kitunguu swaumu
Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au
fanya kutwa mara 2 kama unaumwa na moja wapo ya magonjwa
niliyoyaorodhesha hapa chini.
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa
mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie,
kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna
hii kama wewe ni mjamzito.

Kitunguu swaumu kilichokatwakatwa/chopped
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30
Haya ni baadhi ya magonjwa yanayotibika au kukingika na kitunguu swaumu:
- Huondoa sumu mwilini
- Husafisha tumbo
- Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
- Husafisha njia ya mkojo
- Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria
- Huzuia kuhara damu (Dysentery)
- Huondoa Gesi tumboni
- Hutibu msokoto wa tumbo
- Hutibu Typhoid
- Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
- Hutibu mafua na malaria
- Hutibu kifua kikuu
- Hutibu kipindupindu
- Hutibu upele
- Huvunjavunja mawe katika figo
- Hutibu mba kichwani
- Huupa nguvu ubongo
- Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
- Huongeza SANA nguvu za kiume
- Hutibu maumivu ya kichwa
- Hutibu kizunguzungu
- Hutibu shinikizo la juu la damu
- Huzuia saratani/kansa
- Hutibu maumivu ya jongo/gout
- Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
- Huongeza hamu ya kula
- Huzuia damu kuganda
- Husaidia kutibu kisukari
- Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi
- Huongeza SANA kinga ya mwili
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida
zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa
(ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa
kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
- Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu
(vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa
hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
- Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango
cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
- Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali
iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo
huua fangasi wa aina mbalimbali.
- Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
- Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl
methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa
kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
- Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
- Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
- Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya
seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa
kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya
upasuaji au mara baada ya kujifungua.
- Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
- Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!