KINGUNGE ashauri marais na mawaziri wakuu wastaafu nchini wakutane:;
Mwanasiasa mkongwe nchini KINGUNGE NGOMBALE MWIRU amewashauri marais na Mawaziri wakuu wastaafu nchini kuingilia kati mvutano
Mwanasiasa mkongwe nchini KINGUNGE NGOMBALE MWIRU amewashauri marais
na Mawaziri wakuu wastaafu nchini kuingilia kati mvutano kati ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA na serikali wa kutaka kufanya
mandamano na mikutano nchi nzima bila kibali cha kufanya hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini DSM
KINGUNGE amesema viongozi hao wana nafasi kubwa ya kutafuta suluhu ya
mgogoro huo.
Tayari viongozi mbalimbali wa dini na serikali wameshauri kuwepo kwa maridhiano kati ya serikali na CHADEMA.
Hapo jana Msajili wa Vyama vya siasa nchini jaji FRANCIS MUTUNGI
alitangaza kuwepo kwa kikao tarehe 26 mwezi huu na kisha Baraza la Vyama
vya Siasa nchini tarehe 29 na 30 mwezi huu kwa lengo la kujadili hali
ya kisiasa nchini
CHADEMA imepanga kufanya mikutano na maandamano nchi nzima Septemba Mosi mwaka huu.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani MBEYA limewahakikishia
wananchi wa mkoa huo amani na utulivu katika kipindi cha kuelekea
maandamano yaliyoandaliwa na vyama vya siasa Septemba Mosi mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya BUTUSYO MWAMBELO,
ametoa kauli hiyo baada ya kuhitimisha mazoezi ya kawaida ya Jeshi hilo
ambayo yamefanyika kuzunguka viunga mbalimbali vya Miji ya Mbeya na
Mbalizi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!