Kampuni inayomiliki maduka ya
Kentucky Fried Chicken KFC imeonywa ikome kuchinja kuku waliotibiwa kwa
madawa ya kiuavijasumu au antibiotiki.
Mashirika yanayowakilisha
makundi ya wanunuzi wa bidhaa 350,000 nchini Marekani wamewasilisha
mapendekezo hayo kwa kampuni ya inayomiliki Kentucky Fried Chicken Yum
Brands kufuatia malalamishi kuibuka madawa hayo yanaathiri siha ya
walaji wake.
Tayari KFC imeahidi kupunguza matumizi ya madawa hayo ya binadamu kwa kuku kuanzia mwaka ujao.
Wanaharakati
wanadai kuwa sera nchini Marekani zinaruhusu matumizi ya dosi ya
binadamu kwa kuku jambo ambalo kimsingi linawafanya walaji wa kuku hao
kumeza dozi ya Antibiotiki ambayo hawakukusudia.
Dawa hizo za
antibiotiki hutumika na wafugaji wa kuku ilikuimarisha kasi ya kukua ya
kuku wao iliwatimize vigezo vya uzani na hivyo faida kubwa katika muda
mchache.
Msemaji wa KFC amesema kuwa wanatathmini athari iliyopo
kwa wateja wao kabla ya kutoa vigezo vipya vya kuimarisha ubora wa kuku
watakaowachinja.
Bi Lena Brook wa shirika la wanunuzi la Natural
Resources Defense Council, anasema kuwa KFC sharti ikaze buti kwani
vyakula vyao vinaathiri afya ya wateja wao.
Maduka mengine yanayomilikiwa na Yum , Taco Bell na Pizza Hut
-yanaazimia kupunguza ununuzi wa kuku hao waliotibiwa na antibiotiki.
Juma lililopita maduka ya McDonald yalipiga marufuku ununuzi wa kuku zilizotibiwa na antibiotiki.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!