Mafuta ya nazi ni mazuri kama tu utayatumia ipasavyo, yatakufanya uonekane mrembo, mwenye afya na mwenye ngozi ya kuvutia. Hizi ni baadhi tu ya kazi zake mhimu zaidi mwilini.
1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo
Mafuta ya nazi yana asidi
mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo
mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti
kolesteroli/lehemu
mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa
kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density
Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia
kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu
kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa
Lifesum.
2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito
uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi
kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia
kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza
uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya
kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida.
Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh
Detox. 3. Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi
Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi
kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi
nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka
mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo
mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote
vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa
kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia
unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.
4. Huongeza nguvu mwilini
Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya
kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’
ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini
ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa
‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya
kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi
weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.
5. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya
Tofauti na mafuta ya alizeti
au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi
ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na
viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika
moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata
yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua
au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi
vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!
6. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama
Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni
mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama
mubadala kwa siagi
au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu
mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba
tofauti na mafuta mengine.
7. Huzuia maradhi mengi hatari mwilini
Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo
mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi
kingi cha asidi iitwayo lauric acid.
Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi
hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama
‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi
ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na
kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa
kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mpaka
minne na utaona maajabu.
8. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza
lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo
kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia
kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza
kumbukumbu (Alzheimer).
9. Hutumika kulainisha uke mkavu
Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna
wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa
vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi
katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.
10. Husaidia katika ugonjwa wa aleji
Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza,
moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za
ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na
uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
MHIMU:
Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100,
ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na
kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya
asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi
au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima
utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye
hicho chakula. TAZAMA NAMNA MAFUTA YA NAZI YANAVYOTENGENEZWA
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!