Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imepanga kuanzisha kampeni ya
kuongeza ufahamu kwa watumiaji wa mitandao ili watanzania waepukane na
mkono wa sheria ya makosa ya mitandao inayoelezwa kuwa kikwazo cha uhuru
wa kujieleza
Kampeni
hiyo imekuja mahsusi kwa ajili ya kuimarisha usalama katika matumizi ya
mitandao kipindi hiki ambacho kumekuwa na madai ya watu wengi kukiuka
sheria ya mitandao.
TCRA imeamua kuja na kampeni hiyo kutokana na watanzania wengi kukosa
ufahamu juu ya sheria ya mitandao hali inayochangia uwepo wa ongezeko
la ukiukwaji wa sheria hiyo na kusababisha uwepo wa migogoro.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA James Kilaba amekiri kumekuwa na
ongezeko la watumiaji wa wavuti jambo ambalo linawasukuma kutoa elimu
kwa rika zote ili wafahamu matumizi sahihi ya mitandao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA pia ametumia nafasi hiyo kubainisha
masuala muhimu ya kuzingatia wakati wa kutumia intaneti au mitandao.
Kampeni hiyo inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miezi mitatu na itaendeshwa kwa kutumia mitandao.
COMMENT AND SHARE..................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!