Ni jambo lililo wazi kuwa sote tunakumbana na matatizo , ingawaje aina
ya matatizo na kiwango ambacho yanatusumbua vinaweza kuwa tofauti.
Hata hivyo, sote tunaweza kutafuta mbinu za kutatua matatizo husika,
ingawaje ni kweli mbinu zetu za kutafuta suluhu zinaweza kuwa tofauti.
Katika makala hii kutana na wabunifu Ed na Ross kutoka UK, wanaoendesha biashara yao iitwayo
BUY MY FACE.
Ed na Ross kutoka UK
Vijana hawa walianzisha biashara ya kuuza nafasi za matangazo kwa
kutumia sura zao. Wanachofanya ni kuandika tangazo kwa uso zao, kisha
huzunguka maeneo tofauti tofauti ya mji ili watu waweze kuona tangazo
husika.
Na wameshafanya matangazo ya makampuni makubwa kama vile Ernest & Young.
Jionee picha zao hapa
Mambo kadhaa yanayoweza kukufanya kuwa mbunifu:-
1. Ondoa uwoga: Usiogope kuwa wazo lako litakuja
kushindwa. Chukulia kuwa hata kama litakuja kushindwa, utakuwa tayari
umeshapata uzoefu wa kutengeneza wazo lingine bora zaidi.
2. Usijilinganishe na watu wengine: Usiangalie wengine unao
dhani wamekuzidi uzoefu au ujuzi wamefanya nini , kiasi kwamba
ukajishusha kuwa eti wewe hauwezi kufikia kuwa na kitu kizuri cha
ubunifu.
3. Zingatia Upekee: Kama unataka kufanya UBUNIFU , lakini
mawazoni mwako unapata ukinzani wa kutaka kufanya kama fulani, basi ujue
hapo kuna tatizo. Sisitiza kuwa na upekee, na upekee tuu ndio
utakaoleta maana haswa katika ubunifu wako, hata mbele za wateja. Hata
hivyo hii haimaanishi kuwa hautakiwi kuangalia wengine wamefanya nini,
hapana, angalia wengine kwa lengo la kujifunza, na kutambua mapungufu.
4. Zingatia kukidhi mahitaji ya binadamu: Ubunifu wako hautokuwa
na maana kama haukidhi mahitaji ya watu. Hivyo njia rahisi ya kuanza
ubunifu ni kuisoma jamii, kuangalia matatizo yanayoikumba jamii. Sio
lazima uangalie mbali sana, waweza hata kutafakari matatizo ambayo
yamekuwa yakikutatiza wewe mwenyewe, kisha ukaamua kubuni kitu cha
kuleta suluhisho. Fanya uchunguzi kujua wengine wamekumbana na matatizo
kama yako.
Mfano mzuri,Drew Houston mwanzilishi wa huduma ya kuhifadhi documents online,
DROPBOX anasema alianzisha huduma hiyo baada ya yeye mwenyewe kuwa mpotezaji wa flashdisk wakati akiwa chuoni MIT.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!