JINSI YA KUTUMIA PROGRAMU YA U-TORRENT.
Habari!
Leo ningependa tuzungumzie programu hii ya Utorrent. Watu wengi wamekuwa wakiulizia kuhusu programu hii, inafanyaje kazi na jinzi ya kuitumia katika computer na smartphone.
Tukianza na hili, wengi wamekuwa wakihusisha kazi inayofanywa na Internet Download Manager (IDM) kuwa sawa na ile ya U-torrent.
Hapana! Programu hizi ni tofauti na zimetengenezwa tofauti kabisa. Kwa
mfano IDM huweza kudownload video na mafaili moja kwa moja katika mfumo
wake halisi kutoka katika browser yoyote lakini U-torrent hudownload
video na mafaili yaliyopo katika mfumo wa torrent tu.
U-torrent ni programu iliyoundwa kwa dhumuni la kuwezesha watu
kudownload mafaili makubwa na pia kuweza kukidhi matumizi ya watumiaji
wote wa mtandao. Programu hii huweza ku download file endapo tu
limewekwa katika mfumo wa torrent.
Watu ambao wangependa kugawa au kushea mafaili fulani na wenzao hu
upload mafaili hayo kupitia mitandao maalumu yenye uwezo wa
kuyabadilisha na kuyaweka katika mfumo wa torrent.
JINSI YA KUTUMIA U-TORRENT KATIKA COMPUTER
1. Download U-torrent (Bofya Hapa) au download version mpya zaidi (Bofya hapa).
2. Baada ya kudownload file hilo, INSTALL, unaweza ku double click na kuanza kuliingiza katika computer yako.
3. Baada ya kuinstall U-torrent itafunguka.
Sasa kama nilivyokueleza hapo awali, U-torrent huweza kudownload file
likiwa katika mfumo wa torrent pekee, kwa maana hiyo basi kama file
haliko katika mfumo wa torrent hautaweza kulidownload. Ina maana kama
utaihitaji kudownload nyimbo za Bongo fleva hautaweza kuzipata kwa
kutumia U-torrent kwani watu hawajaziweka katika mfumo huo.
Hatua inayofuata baada ya kuinstall U-torrent katika computer yako ni
kutafuta faili unalohitaji kulidownload ambalo lipo katika mfumo wa
torrent. Kwa bahati nzuri kama unatumia Mozilla Firefox hukuwezesha
kudownload torrent haraka zaidi pindi unapoifungua. Utatumia njia za
kawaida kama unazotumia wakati unapohitaji kusearch file kupitia google
sema sasa itabidi tutumie google ambayo ina mafaili ya torrent tu.
Google hizi zenye torrent tu ni hizi hapa:
Ninakushauri utumie
www.kickass.to kwa sababu ya mpangilio wake mzuri.
4. Baada ya kufungua search engine hiyo au google hiyo unaweza sasa
kusearch kile unachotaka kudownload. Kwa mfano kama tunahitaji
kudownload programu ya Ashampoo Burning Studio. Itakuwa kama hivi.
5.Katika matokeo utakayoyaona utachagua lile ambalo ni bora kwa matakwa yako. Kisha fanya kulibonyeza.
6.Baada ya hapo bonyeza kitufe cha DOWNLOAD TORRENT. Kama unatumia
Mozilla firefox utaona baada ya kubofya kitufe hicho ujumbe unaokuuliza
kama unahitaji kusevu kwa U-torrent sema OK kisha fuata hatua ifuatayo.
Kama unatumia Chrome au Firefox na haujaona ujumbe huo, fungua tu
U-torrent kisha tizama upande wa juu kushoto na chagua alama ya
kujumlisha (+). Baada ya hapo chagua file unalotaka kulidownload kutoka
katika Downloads litakuwa na picha kama hii na jina la programu hiyo
pia.
7.Baada ya hapo utaweza kuchagua ni kipi ungependa kuchukua na kipi
usingependa kuchukua katika file husika. Usichague kama hauna uhakika.
Baada ya hapo bofya OK. File litaanza kudownowload.
Hongera umejifunza jinsi ya kutumia U-torrent kudownload mafaili mbalimbali.
PS: Nimetumia neno
Google
ya Torrent ili kurahisisha msomaji kuelewa kuwa zile tovuti hufanya
kazi ya ku search kama google lakini hazina uhusiano wowote na google.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
You liked it....,
ReplyDeletegood
ReplyDelete