Jifunze Haya Wewe Mwanamke Uliye Single:;
1- Kamwe usisahau kumuomba Mungu wako kabla hujasema "YES" kwa yule
unaedhani anapaswa kujenga maisha na wewe. Usikimbilie kuolewa. Kama
utakimbilia kuolewa, utaikimbia ndoa na tena kwa majeraha makubwa.
2- Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa. Fanya biashara yoyote,
tafuta shughuli ya kufanya. Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza
maisha. Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako.
3- Usimkimbilie mwanaume kwa sababu ya pesa zake, magari, connection,
cheo, kipaji, ucheshi, au background ya familia yake. Olewa na mwanaume
aliye na hofu ya Mungu. Hapo utakua umekula BINGO...!
4- Jenga tabia ya kula vizuri kwa afya. Usile alimradi umekula. Kula
vyakula vya kujenga mwili na uwe mlo kamili. Fanya mazoezi mara kwa mara
kuepuka unene usio wa lazima.
5- Vaa vizuri. "first impression counts" hii inamaanisha kwamba
muonekano wa mwanzo unamaana sana kwa mtu atakayekuona. Usiache maeneo
yako ya siri yakaonwa na mwanaume yeyote, vinginevyo utawavutia wale
wanaume wakware ambao sio waoaji.
6- Usililie au kulazimisha mwanaume akuoe. Wewe ni wa thamani mno
kufanya hivyo. Usilazimishe ndoa kwa kumbebea mimba, wenzako wamefanya
hivyo na leo wengi wao wanajuta. Wamebaki wakilea peke yao.
7- Tabia yako ndio Ndoa yako. Hiyo ndio itakayoamua mwanaume aishi na
wewe au laa. Jitathimini tabia yako. Uzuri sio kila kitu, kama
unajivunia na uzuri wako na unaamini kama ndio utakaokupa mume utapoteza
nafasi yako kwa aliye mzuri zaidi yako kwa tabia na sura.
8- Usichoke kujifunza kupika, kujua kupika wali, ugali, mboga na chapati
haitoshi. Jifunze zaidi, tizama vipindi vya mapishi, soma vitabu
mbalimbali vya mapishi, tembelea page mbalimbali zinazofundisha kupika
vyakula aina mbalimbali.
Wanaume mara nyingi wanapenda wanawake wanaojua kupika, wale ambao kila
siku wana suprise ya aina mpya ya mapishi. Kwa sababu njia nyingine
rahisi ya kutambua moyo wa mwanaume ni kupitia tumbo lake (chakula
kizuri)
9- Usiishi kwa mazoea utakapoolewa, soma vitabu vya mahusiano, ndoa na
familia. Ongea na wazazi wako na wazee wengine wakupe busara zao.
Kupitia kwao akili itaweza kupanuka na kupata ufahamu wa nani haswa
atapaswa kuishi na wewe.
10- Acha ushabiki kwenye mitandao ya kijamii mambo ya Team Zari, Team
Wema, Team Chura, na mengineyo hayatakusaidia. Wenzako wana maisha yao,
muda huo tumia kuhudhuria semina mbalimbali za ndoa, tembelea washauri
wa mahusiano na ndoa.
Msome Chriss Mauki, Tweve Hezron, Eliado Tarimo, Prince Naahjum Alsina
na wengineo kwa dondoo mbalimbali za mahusiano, kupitia huko ufahamu
wako waweza kuongezeka kwa kiasi fulani, hii itaepusha sana kuja kuishi
kwa mazoea.
******************
Ni hayo tu sina la ziada, Binafsi wanawake nawakubali sana, sijui
kwanini...!? labda kupitia ujasiri wa mama yangu. Ninafahamu kupitia
ninyi tunaweza tukawa na familia bora ambako huko ndiko maadili ya taifa
huanzia.
Heshima ya mwanamke ni NDOA, heshima ya mwanaume ni MAJUKUMU.
Life is full of joy, Enjoy it!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!