JE NI UMRI GANI MUAFAKA WA KUPIMA SARATANI YA TEZI DUME?:;
Saratani ya tezi ya prostate(tezi dume) ni ile ambayo seli zisizo za
kawaida hukua katika tezi ya prostate iliyopo katika mfumo wa uzazi wa
mwanaume. Kwa walio wengi, ukuaji wa saratani hii huwa ni wa taratibu ingawa
kwa wengine yaweza kukua kwa haraka. Saratani yaweza kusambaa katika sehemu nyingine
za mwili,hususan katika mifupa na tezi zinazo husika na kinga ya mwili (lymph nodes).
Mara nyingi saratani ya
tezi ya prostate huwa haionyeshi dalili yeyote katika hatua za awali.
Saratani hii imeonekana kuwaathiri zaidi wanaume wenye asili ya Afrika
na Caribbean lakini haijulikani ni kwa sababu gani.
Dalili za saratani hii hutofautiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine;
baadhi ya wanaume huwa hawaonyeshi dalili hadi saratani inapokua baada ya mwaka
mmoja, na dalili zinapojitokeza huwa kama ifuatavyo:
- Kukojoa mara kwa mara
- Mkojo unaokatika wakati wa kukojoa.
- Mkojo kutoka kwa shida unapoanza kukojoa.
- Damu katika mkojo au katika majimaji yanayobeba
mbegu za kiume.
- Maumivu wakati wa kukojoa au kujamiaana.
- Maumivu makali ya mgongo, kiuno mapaja, hususan
pale ugonjwa unakua umesambaa katika ogani nyingine za mwili.
Kuna aina mbili za magonjwa ambazo husababisha dalili zinazofanana na
saratani ya tezi ya prostate. Ugonjwa wa kwanza ni ule ambao tezi ya prostate
huongezeka ukubwa isivyo kawaida, lakini ukuaji huu hausababishwi na saratani
(kitaalam hujulikana kama benign
prostatic hyperplasia- BPH). BPH husababisha dalili kwa kuongeza mkandamizo
katika kibofu cha mkojo, mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu, au kibofu
pamoja na mrija kwa pamoja na ugonjwa huwapata wanaume wenye umri mkubwa.
Ugonjwa wa pili ni ule ambao husababishwa na uambukizi katika tezi ya prostate
na kupelekea uvimbe wa tezi hii. Magonjwa haya yote hutibika na BPH wakati
mwingine huitaji matibabu ya upasuaji.
Watafiti wanashauri watu kutumia vyakula kama matunda na mboga mboga
kwa kuwa vyakula kutokana na wanyama kwa wingi, kama nyama zenye mafuta mengi
ni vichochezi vinavyoweza kusababisha mtu kupata saratani ya tezi ya prostate,
ingawa tafiti zaidi zinaendelea kujua ni kwa jinsi gani vyakula hivi
vinachochea mtu kupata ugonjwa huu.
Je saratani ya tezi dume yaweza
kugundulika mapema?
Ijapokuwa upimaji wa saratani ya tezi dume huwa haufanyiki mara kwa
mara na huwa hamna kampeni za kuhamasisha upimaji kama ilivyokuwa kwa saratani
ya matiti, lakini wataalam wanaohusika na magonjwa ya saratani wanashauri
upimaji wa saratani kwa makundi yafuatayo:
- Wanaume wenye miaka 50 na wanataka kuongeza umri
wa kuishi.
- Wanaume wenye miaka 45 wa asili ya Afrika wenye
baba au kaka ambao walipatikana na saratani ya tezi ya kiume kabla ya miaka 65.
- Wanaume wenye miaka 40 ambao ndugu wa karibu
(baba, kaka au kijana) walipatikana na saratani ya tezi ya prostate katika umri
mdogo.
Vipimo vya awali kabisa ili kugundua ugonjwa huu hujulikana kama PSA (prostate specific antigen) na kingine ni
DRE (digital rectal examination)
ambapo daktari hutumia glove kwa kutumia kidole kupitia njia ya haja kubwa
kupapasa uvimbe katika tezi ya prostate. PSA ni kwa kupima damu kuangalia
kiwango cha antigeni za prostate. Daktari na mgojwa hutakiwa kuwa makini kuhusu
majibu ya vipimo hivi kwa kuwa ni vipimo vya awali kabisa na matokeo yaliyo
chanya hayamaanishi mojakwamoja kuwa mgonjwa anayo saratani. Daktari atamsaidia
mgonjwa kuamua ni nini maana ya vipimo vyote vya PSA na DRE na kuamua vipimo
vitakavyofuata baada ya vipimo hivyo.
Kama daktari wako ataamua kuwa vipimo vya PSA na DRE vimeonyesha
saratani ya prostate, kipimo kitakachofuata ni upimaji wa tishu kutoka katika
tezi ya prostate ( kitaalam kama biopsy).
Kipimo hiki hufanyika kwa kuchukua tishu kwa kutumia sindano maalum, ambapo
tishu hizi huchunguzwa kwa kutumia darubini ili kuangalia uwepo wa seli za
saratani katika tezi ya prostate.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!