"Moja nimekuja kuwashukuru na kuwaeleza
tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Mimi
, nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa hizo kura milioni 6
wakazuia mikutano ya hadhara haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia
ninayotaka kuhudhuria ,wanatisha wafanyabiashara wanatukodisha kumbi za
mikutano wanateseka kweli kweli.
CHADEMA chama chetu ni kikubwa
sana , kinawatesa sana , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015,
tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu kweli kweli
, wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya
wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni wapinzani .
Pili
Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na
wanajua sisi ni wamoja . Mkutano mkuu CCM kule Dodoma walinitaja Mara
360 na zaidi , mkutano ule ulikuwa wa Lowassa kwa kuwa wanateshwa na
jinamizi langu , linawatesa kweli kweli , kule nimetoka na CCM haipo
tena nimeacha Lowassa na ndio sababu wanapata tabu kwa kuwa wanajua
tumewashinda nchi hadi ndani ya chama chao.
KUHUSU UKUTA .
Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si
jambo dogo hata kidogo ,Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia
wake wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi
nina hofu kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae.
Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .
Wasuluhishi wanasema tuzungumze ,
tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba
na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa. Mtu mmoja anajiamulia
kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi
hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo
yake .
POLISI niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi
kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri
tutadeal nao mmoja mmoja, hatutodili na jeshi tutadili Na Polisi
aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC . Ni
bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji
wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
Tabia
za viongozi Wa kiafrika ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga
demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee hata kidogo litokee
Tanzania. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue
jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na
haki za kidemokrasia .
Tujitokeze kwa wingi sana September 1,
tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa
kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu . tuna chama
Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na
ustawi wa nchi .
Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni kwa kunisikiliza."
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!