Hamisa Mobetto Aukata Mzizi wa Fitina Kuhusu Tetesi za Kutoka na Diamond:;

Kwa muda sasa mlimbwende wa Tanzania, Hamisa Mobetto amekuwa akituhumiwa
kutaka kumpindua Zari the Bosslady kwa Diamond Platnumz.
Skendo hizo zilivuma zaidi mwezi na kitu uliopita baada ya kudaiwa kuwa
uwepo wa mrembo huyo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Diamond
kulitaka kusababisha timbwili kwakuwa Zari alikuwepo.
Na sasa Hamisa amefunguka kuwa yeye na Diamond hata hawajuani kihivyo!
“Hiyo sio kweli,” alisema Hamisa kwenye mahojiano na gazeti la The Citizen baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo.
“Pia sijawahi kuwa karibu na Diamond na siku ya kwanza tumekutana
ilikuwa ni siku anazindua video ya Number 1 pale Serena,” aliongeza.
“Tena wakati hiyo habari imeanza kusambaa nilikuwa nje ya nchi.”
Habari hizo zilivuma zaidi wiki kama tatu zilizopita baada ya kuonekana
picha ya Hamisa akiwa kwenye chumba kile kile Diamond alilala na Zari
Afrika Kusini.
Diamond alilazimika kutolea ufafanuzi picha hizo kupitia kipindi cha Leo
Tena cha Clouds FM. Pia alielezea tetesi za kuwa na uhusiano na mrembo
huyo.
“Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na
yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny
na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo,” alisema Diamond.
Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja
alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment
ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia
ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi
tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!