Goodluck Jonathan: Waasi wa Niger Delta wanataka kuniua
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Rais mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kuwa waasi wa Niger Delta wanataka kumuangamiza.
Kupitia
kwa taarifa iliyochapishwa na msemaji wake rais Jonathan anasema kuwa
madai ya kuwa ndiye anayewafadhili waasi wa Niger Delta Avengers ambao
wameshambulia muundo msingi wa uchimbaji mafuta katika eneo lao katika
siku za hivi punde.
Wapinzani wake wanadai kuwa rais huyo
aliyeondoka madarakani mwaka uliopita huenda anapanga njama na waasi hao
ilikuihujumu serikali iliyoko sasa.
Taarifa hiyo inasema kuwa madai hayo yote ni ya porojo.
''Mimi mwenyewe nimelengwa katika mashambulizi kadha
yanayolenga kuniua haswa na kundi la Mend (Movement for the Emancipation
of Niger Delta )
''sio ukweli kuwa wale waliotaka kuniua sasa
ndio wandani wangu''Mimi mwenyewe nimelengwa katika mashambulizi kadha
yanayolenga kuniua haswa na kundi la Mend (Movement for the Emancipation
of Niger Delta )
Waasi hao wa Niger Delta Avengers wametatiza
kabisa shughuli ya uchimbaji mafuta kwa mashambulio ya mara kwa mara
kwenye muundo msingi wa mafuta katika jimbo la Niger Delta.
Wanasiasa na wapiganiaji haki za wenyeji wa eneo la mdomo wa mto
Niger, wamelalamika kuwa jamii za Niger Delta, zinastahiki kupewa
utajiri unaotoka eneo lao, na wanataka uchafu kutoka visima vya mafuta,
usafishwe.
Majuzi tu rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, aliahidi
kuwa ataendelea na mpango wa kuwasamehe wapiganaji walioshiriki uhasama
dhidi ya serikali.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!