FANYA YAFUATAYO UWE NA AFYA NJEMA:;
1.Kunywa kiasi cha kutosha cha maji
safi na salama baada ya mazoezi au kazi iliyokufanya utoke jasho na
epuka unywaji wa vinywaji baridi kama soda. Unywaji wa maji utasaidia
mwili kurudisha maji na madini yaliyopotea mwilini. Maji ni muhimu
katika ufanyaji kazi wa mifumo mbali mbali ya mwili.
2.
Jifunze kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo vya mwili unapoamka, hii husaidia kuboresha
mzunguko wa damu, mmeng'enyo na kukusaidia kuondoa maumivu ya
viungo.
3.Kamwe usianze siku yako bila kifungua kinywa. Tafiti zinaonyesha kuwa,
kifungua kinywa sahihi ni muhimu hususani kwa wale wanaotaka kupungua
uzito. Wale wasiopata kifungua kinywa asubuhi wanakua katika hatari ya
kuwa na uzito mkubwa. Mlo kamili kwa kifungua kinywa ni kama juisi za
matunda, mkate wa ngano isiyokobolewa, mboga mboga, maziwa, mayai na
maji.
4.Usitumie vyakula vyenye wanga kabla ya saa moja kupita baada ya
mazoezi. Hii itaulazimisha mwili wako kuanza kutumia kiasi cha mafuta
yaliyohifadhiwa mwilini badala ya kutumia chakula ulichokula. Unaweza
kula matunda katika muda huo ila epuka vinywaji kama bia au soda.
5.Tumia vyakula vyenye Vitamini C kwa wingi, miili yetu huitaji angalau
kiasi cha 100mg za Vitamini C kwa siku. Njia bora ya kufikia kiwango
hiki ni kadiri ya milo mitano kwa siku ya matunda pamoja na mboga mboga
zenye Vitamini hii. Mfano wa vyakula vyenye Vitamini C ni Chungwa,
zabibu, pera, embe na mboga za majani.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!