FAIDA ZA PARACHICHI:;
Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana. Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka
jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale
kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo
la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo
kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe
sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.
Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine,
kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate)
kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.
Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za
parachichi.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
7ug
|
|
Vitamini E
|
2.1ug
|
|
Vitamini C
|
10mg
|
|
Thiamine
|
0.1mg
|
|
Niacini
|
1.7mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.3mg
|
|
Folic acid
|
81ug
|
Madini
|
Kalshamu
|
12mg
|
|
Phosphorasi
|
52mg
|
|
Magnesiamu
|
29mg
|
|
Potasiamu
|
599mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
7mg
|
|
Chuma
|
0.6mg
|
|
Zinki
|
0.6mg
|
|
Shaba
|
0.2mg
|
|
Manganizi
|
0.1mg
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
25mg
|
|
THR(Threonine)
|
73mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
84mg
|
|
LEU(Leucine)
|
143mg
|
|
LYS(Lysine)
|
132mg
|
|
MET(Methionine)
|
30mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
27mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
232mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
49mg
|
|
VAL(Valine)
|
107mg
|
|
ARG(Arginine)
|
88mg
|
|
HIS(Histidine)
|
49mg
|
Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya
ya moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta
ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo
kitaalam kama polysaturated fat), na
kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat). Parachichi ni chanzo
kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu. Utafiti unaonyesha kuwa
matumizi ya mafuta haya katika parachi hupunguza lehemu
iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density
lipoprotein), na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density lipoprotein).
Madini ya Potasiamu ni aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha
kutoka katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium
kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya
huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu, shinikizo la juu la damu laweza
kupelekea mtu kupata kiharusi, shambulizi la moyo hata figo kushindwa kufanya
kazi.
Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka
katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa
zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia
urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata
magonjwa mengi mwilini. Kuna aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa
ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na
kusaidia mwili kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi
lina kiwango kikubwa cha fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali ya kawaida.
Aina ya mafuta na virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi vinasaidia afya ya
ngozi yako. Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa na unyevu unaotakiwa na
kuifanya ngozi kuwa laini na yenye afya. Vitamini C husaidia katika kusaidia
uponaji haraka wa ngozi na kujijenga upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia
kujenga elastini na collageni ambazo ni muhimu katika ngozi.
Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants)
katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na
mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi
yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.
Tunda hili ni lishe bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina
kiwango kidogo cha sukari ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa mafuta
aina ya ‘monosaturated’ husaidia
kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango
cha sukari mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C katika parachichi husaidia kuimarisha mishipa
ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida kubwa kwa wagonjwa wenye
kisukari.
Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina
Vitamini E ambayo ni “antioxidant” Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo
hutusaidia kutukinga na magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile
kinachosaidia afya ya moyo pia husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa
ya moyo na kisukari huwa tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.
Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya
ya macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja
uko Marekani, ulionyesha kuwa watu walao parachichi walionekana kuwa na
afya bora
ukilinganisha na wale wasiokula parachichi. Waliokula parachichi
hawakupatwa na matatizo ya mmeng’enyo ukilinganisha na
wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya
moyo na kisukari.
Unasubiri nini sasa? Anza kutumia matunda haya kuboresha afya yako.
Unapokwenda sokoni usisahau kununua parachichi.Faida ni nyingi zitokanazo na
ulaji wa tunda hili.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!