Ndoa
ni muungano wa watu wawili wenye nia ya kuishi pamoja pengine kwa
maisha yao yote. Ni muungano wenye malengo ya kujenga familia pamoja na
kuiongoza kwa namna ambavyo itakuwa bora kwao.
Utafiti unaonyesha kuwa kuna faida za kuwa katika ndoa kiuchumi na kiafya. Watu walio katika ndoa huwa na afya njema na pia huwa na maendeleo zaidi kiuchumi ukilinganisha na wale ambao wanaishi peke yao.
Watu ambao wapo katika katika ndoa wana nafasi ndogo ya kupata magonjwa ya moyo kwa 5% ukilinganisha na wale ambao hawako katika ndoa ambao wana hatari kwa 3% zaidi ya kupata magonjwa hayo.
Hali kadhalika wale ambao wako katika ndoa wananafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi ya maendeleo kuliko watu wawili ambao hawako katika ndoa. Hii inasababishwa na mtindo wa maisha ambao wasio katika ndoa wanaishi. Vitu kama ulaji mbaya,ulevi usio na mipaka na matumizi mabaya ya fedha zao.
Faida za Kuwa Katika Ndoa Kiafya
Kwa wastani utafiti unaonyesha watu ambao wako katika ndoa wanaishi maisha marefu yenye afya na furaha zaidi kuliko wale wasiokuwa katika uhusiano ya ndoa.
Wanaume wanaume ambao hawana uhusiano wa ndoa
wanakawaida ya kula vibaya vyakula visivyo na faida kiafya.Baadhi yao
wanakuwa walevi na matumizi yao ya fedha yanakuwa makubwa.
Kwa kuwa hawapiki nyumbani, hula sehemu za jumuia kama mikahawani na
katika vilabu vya pombe. Vyakula hivi havina mchanganyiko mzuri wa
virutubisho vinavyohitajika katika mwili.
Wanawake wasioolewa nao ulaji wao wakati mwingi unakuwa wa kula nje
japo si kama wanaume,lakini pia wanakula vibaya vyakula vyenye mafuta
mengi na visivyo na virutubisho muhimu. Vyote katika hivi vinapelekea
kuhatarisha afya zao.
Wanawake na wanaume ambao wameachana au mwenza wao amefariki
wanazongwa sana na upweke wa kihisia. Hili hupelekea kupata magonjwa
yanayosababishwa na msongo wa mawazo.
Uzalishwaji wa kemikali ya
endorphin ambayo inafanya kazi ya
kutuliza maumivu mwilini na kumfanya mtu awe mwenye furaha unakuwa wa
kiasi kidogo na hivyo kukumbwa na matatizo ya kiafya na kihisia.
Imefahamika kuwa wanawake na wanaume wasio na ndoa
wanakuwa na hasira na wakali sehemu za kazi na kwa watu wengine
wanaokutana nao,na wanakuwa wagumu kuelewana na watu katika mahusiano ya
kikazi au jumuiya nyingine.
Faida za Kuwa Katika Ndoa Kiuchumi

Kuna faida nyingi zinazotokana na watu kuwa katika ndoa ambazo huleta mafanikio kiuchumi
i. Matumizi Machache:
Tumeona kuwa watu wasiokuwa katika ndoa hula chakula nje zaidi na kunywa vilevi, hivyo hutumia fedha zaidi kwa mambo yasiyo ya msingi hasa kwa wanaume.
Wanawake hali kadharika hutumia fedha nyingi katika mavazi na vipodozi wakiwa hawako katika ndoa kuliko wale walioolewa.
ii. Malengo ya Muda Mrefu:
Mipango ya watu wasio katika ndoa
huwa ni ya muda mfupi na starehe zaidi hivyo kufanya maendeleo yao
kiuchumi kuwa chini. Kinyume chake ni kuwa wale ambao wako katika
mahusiano hupunguza matumizi kwa kula nyumbani zaidi na kupunguza
matumizi katika vitu visivyo vya muhimu kama mavazi ya fahari.
Malengo ya watu waliooana huwa ya kujenga familia na ni malengo ya
muda mrefu. Badala ya kufanya starehe kupita kiasi huwekeza katika
ujenzi na biashara ambazo zitaongeza kipato chao.
iii. Kipato Kikubwa:
Kipato chao pia huongezeka kwa kuweka nguvu pamoja. Kama wote ni
waajiriwa basi kutakuwa na mishahara miwili mwisho wa kila mwezi badala
ya mtu mmoja na hivyo uwezo wao wa kufanya mambo makubwa unaongezeka.
Watoto wanapozaliwa katika familia huongeza mahitaji ya familia na ghrama huongezeka. Kwa kuwa inasemekana kuwa “
uwezo wa binadamu kufikiri hukua kutokana na tatizo” wazazi walio katika ndoa
hupata jinsi nyingine ya kuongeza kipato na hivyo kukua kiuchumi.
Watafikiria miradi zaidi au hata kutafuta kazi inayowalipa zaidi.
Hitimisho:
Ni wazi kuwa kuna raha ya kuwa na mtu unayempenda katika maisha yako na kujenga naye familia. Kama ndoa
yenu ina furaha ni wazi utakuwa mtu mwenye furaha; na inajuliknana kuwa
mtu mwenye furaha huishi maisha marefu na huwa na afya nyema.
Hali kadhalika walio katika ndoa wana wajibika zaidi kuliko wale wasio katika ndoa na huweka jitihada za ziada za kujiongezea kipato. Hivyo uchumi wa walio katika ndoa huimarika zaidi na kuwafanya waendelee kwa haraka.
Lakini ifahamike kuwa hili linawezekana tu kama ndoa yao ina furaha, ikiwa vinginevyo matokeo huwa kinyume chake.
COMMENT AND SHARE....................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!