FAIDA YA KUSHIRIKI MICHEZO NI ZAIDI YA KUJENGA MWILI:;
Tutakubaliana
kuwa hali ya michezo nchini inazidi kudorora hasa ukiangalia wanafunzi wa shule
za awali pamoja na upili na hata vyuo vikuu, ushiriki wa michezo sio kama miaka
ya nyuma. Ingawa wanamichezo wanaweza kuumia wawapo michezoni lakini hiyo siyo
sababu ya kumzuia mtu asishiriki michezo, na faida ni kubwa sana itokanayo na
michezo, na kuumia michezoni kwaweza kuepukwa kwa kuchukua tahadhari.
Faida za
michezo ya ushindani (mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mbio za miguu,mbio za
baiskeli,tenisi nk) ambayo hupelekea mazoezi ya viungo ziko wazi kabisa. Ni
wazi pia matatizo ya kuwa na uzito mkubwa (obesity) yanaongezeka kutoka na
mfumo mpya wa maisha ukilinganisha na miaka ya nyuma. Ingawa uzito wa wastani
kiafya kwa wanamichezo husaidia katika ufanisi wa michezo hiyo, hiyo siyo faida
pekee itokanayo na ushiriki katika michezo mara kwa mara. Miongoni mwa
wanamichezo siyo rahisi kupata magonjwa ya kisukari, shinikizo kubwa la damu,
na pia kujengeka katika hali ya afya njema ya viungo mbalimbali vya mwili, afya
ya akili huimarika, ambapo yote hayo hupelekea kuwa na jamii ya watu wenye afya na
furaha.
Lakini, faida
ya michezo siyo tu kujengeka kwa mwili wenye afya bora.
Zifuatazo sababu chache kwa nini
unatakiwa ushiriki katika michezo au kuwatia moyo watoto wetu washiriki katika
michezo mbalimbali.
Sababu za kijamii.
Tafiti mbalimbali
zinaonyesha kuwa, watoto na vijana wanaoshiriki katika michezo mbalimbali
katika shule za awali, za upili hata vyuo vikuu, huwa hawajihusishi kwa wingi katika
matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, sigara na vitendo vya ngono
ikilinganishwa na wale ambao hawajihusishi au kushiri katika michezo mbali
mbali. Tafiti pia zimeonyesha wanafunzi wa kike wanaojihusisha na michezo
katika shule za upili ni wacheche sana hupata mimba wakiwa katika masomo
ukilinganisha na wale wasioshiriki katika michezo.
Maendeleo ya
kielimu.
Michezo ambayo hupelekea mazoezi ya mwili ni njia
nzuri ya kujenga afya ya akili.Watoto na wanafunzi wanaoshiriki katika michezo,
huwa na hamu ya kula, hupata usingizi vizuri,kinga ya mwili huimarika, hukua
wakiwa wachangamfu wenye afya na miili yenye nguvu, pia afya ya akili huimarika
maradufu ukilinganisha na wale wasioshiriki katika michezo. Katika utafiti
mmoja uliofanyika huko Colorado Marekani, ulionyesha kuwa, wanafunzi waliokuwa
washirika katika michezo, walionyesha mafanikio makubwa darasani na kuwa na
matokeo yaliyotia moyo. Pia michezo itawajengea wanafunzi ujuzi katika uongozi,
ujuzi ambao utawasaidia mbeleni maishani mwao.
Kazini.
Utendaji na ufanisi kazini, utategemea na afya za
wafanyakazi katika sehemu zao za kazi, michezo ni chombo kinachoweza kuongeza
ufanisi kwa kuboresha afya za wafanyakazi. Wengi haitawaingia akilini
nikiwaambia kuwa michezo inaweza kuongeza kipato cha wafanyakazi, kuwawezesha
kupata cheo, kupata kazi nzuri, kuongeza ujuzi katika uongozi, kumuongezea
mfanyakazi uwezo kufanya kazi kama timu na kujenga ushirikiano mzuri na
wafanyakazi wengine wa kampuni moja na hata kampuni nyingine.
Mpe moyo mtoto
wako kushiriki katika michezo.
Wazazi wanaweza kuwasaidia watoto wao kuwa wachangamfu
na wenye afya kwa njia mbalimbali ikiwemo:
o
Kuongoza kwa mfano halisi, mzazi mwenyewe awe
mshiriki wa michezo ili kuwa mchangamfu, mwenye nguvu na afya.
o
Hakikisha familia mnapotoka muwe na wakati wa
michezo, au kushiriki michezo mbalimbali pamoja.
o
Mshawishi mwanao kutembea au kuendesha baiskeli
kwa safari fupi, kuliko kutegemea kupelekwa kwa gari au kutumia usafiri wa
umma.
o
Msapoti mwanao katika juhudi zake za kushiriki
katika michezo. Ikiwezekana uwepo wakati wa mechi mbalimbali za michezo
anazoshiriki, ukiwashangilia kama mshabiki wao.
o
Panga muda wa mtoto wa kuangalia televisheni,
kompyuta au kucheza michezo mbalimbali ya komputa.
o
Wasiliana na walimu wa shule yake kuangalia
uwezekano wa kumshawishi kushiriki michezo mbali mbali.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!