Licha ya jamii kutegemea sana kupata taarifa mbalimbali kutoka vyombo
vya habari vya magazeti, msanii Diamond Platnumz ameonekana kutokuwa na
imani na vyombo hivyo hususani magazeti ya udaku kiasi cha kuwaasa
mashabiki wake.
Akiongea
kwenye mahojiano na runinga ya EATV kwenye kipindi cha eNewz Diamond
Platnumz amewaambia mashabiki wake wasiamini kila kinachoandikwa na
magazeti kinachomhusu yeye na maisha yake ya kila siku kwani mambo hayo
hayana ukweli, na wala kwa sasa hafanyi mahojiano na gazeti lolote.
Diamond ameendelea kusisitza wananchi wafuatilie mitandao ya kijamii
kama vile Instagram, facebook, twitter, na snapchat kwani kila
kinachokuwa pale kina muhusu asilimia mia moja.
Pamoja na mambo mengine Diamond ameeleza kuwa mara ya mwisho kafanya
mahojiano na waandishi wa magazeti ni siku alipokuwa akizindua label
yake ya WCB.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!