Msanii Diamond Plutnuz amewashangaza watu baada ya kauli yake kwamba
anaona bifu kwenye muziki na kitu kizuri, tofauti na wasanii wenzake
wengi ambao hupinga suala la bifu.
Diamond amesema kwake yeye
anaona ni sawa tu iwapo wasanii wanakuwa na bifu, kwani inasaidia kwa
kiasi kikubwa kuinua muziki wao, kwa kuzungumziwa na vyombo vya habari
na watu mbali mbali, isipokuwa inakuwa shubiri pale inapogusa familia,
na kutoleana maneno machafu.
"Bifu mi naona fresh, kwangu kitu kikizungumziwa ndo naona poa tu
kwanza inaniongezea, ila pale inapofikia kugusa kwenye familia na
kutoleana maneno machafu ndio inakuwa sio poa", alisema Diamond
Plutnumz.
Kutokana na kauli hiyo, Diamond amekuwa amepigia mstari kuwa wasanii
wa lebo yake ya WCB hutegemea 'kiki' zaidi kuliko kazi bora kuweza
ku-hit, kama ambvyo watu wengi huwatuhumu wasanii hao.
Pia Diamond ametoa siri kuwa mashabiki wake wajiandae mkao wa kula
kwani kabla mwaka huu kuisha, atatoa album ambayo itakuwa ya kimataifa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!