Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I:;
U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘
Urinary tract infections’,
ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa
unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia
wanapatwa na ugonjwa huu. Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa
huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.
Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo
mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja
ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo
utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra.
Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu
nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.
Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza
kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.
Kinachosababisha U.T.I:
- Kisukari
- Maumivu ya mishipa
- Ajari katika uti wa mgongo
- Ushoga (kwa wanaume)
- Usafi duni
- Upungufu wa maji mwilini
- Kushikilia mkojo muda mrefu
- Kurithi
- Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.
Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I
- Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
- Kukojoa mara kwa mara
- Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
- Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
- Mikojo kukutoka pasipo kutaka
- Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
- Kukojoa damu
- Harufu nzito au mbaya ya mkojo
- Homa
- Kusikia baridi
- Kutokujisikia vizuri
- Kujisikia uchovu
Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I
1. Baking Soda

Baking Soda
U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa
daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi
kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi. Ili kuzuia U.T.I
isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking
soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au
kuendela kwa maambukizi ya U.T.I. Baking soda itapunguza hali ya uasidi
katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka. Baking soda ni ile
kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko
kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.
2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):

Zabibu nyeusi

Zabibu nyekundu
Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo
zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti
bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa
na uwezo wa kudhibiti U.T.I. Pendelea kutumia juisi ya matunda haya
glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na
ugonjwa huu.
3.
Nanasi

Nanasi
Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti
maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu
sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘
Bromelain’.
Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba
na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I. Kula
vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na
ugonjwa huu.
4. Maji

maji
Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara
kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau
glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo
hayajawekwa kwenye friji. Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu
wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya
njano. Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria
wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili
kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo
ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya
mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa.
5. Vitamini C

Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini
Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C
kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara
kwenye njia ya mkojo. Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya
kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu
katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo.
Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye mlonge. Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.
6. Kitunguu swaumu:

Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu
maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria na
virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na
hata ile ya kibofu cha mkojo. Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu
ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I.
Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2,
menya nusu yake (punje 10 au 15), menya punje moja baada ya nyingine na
kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama
unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na mapema
uamkapo asubuhi kwa siku 7.
7. Limau/ndimu:

Limau/Ndimu
Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limau au ndimu na uongeze
maji ili kupata robo lita (ml 250) na unywe kutwa mara tatu. Pia unaweza
kuongeza asali
vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya
uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia
kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu
cha mkojo.
8. Unga wa majani ya Mlonge

Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji, au ndani ya juisi ya
matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au
katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo
lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa
mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali. Tumia kwa mwezi mmoja
mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa.
9. Mshubiri (Aloe-Vera):

Mshubiri/Aloe Vera
Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa vinne, changanya na maji
ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya
vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 2 au
hadi utakapopona. Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa
vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.
Katika dawa hizi zote zilizojadiliwa hapa, napendekeza utumie dawa
hizi kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na kwa haraka, nazo ni; maji
ya kunywa, kitunguu swaumu, limau, unga wa majani ya mlonge na mshubiri.
Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I
- Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
- Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
- Penda kuwa msafi.
- Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
- Pata haja ndogo mara baada ya tendo la ndoa.
- Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda
- Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
- Epuka kaffeina.
- Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Dawa mbadala hizi 9 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I
au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu
au dalili zinadumu kwa muda mrefu.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!