Dalili za Ndoa Inayokufa:;
Jitahidi kuhakikisha unalinda moyo wako na moyo wa mpenzi wako; usije ukaupasua na kuuumiza.
Wanandoa wengi hujikuta wamefika mahali
ambapo ndoa haiwezi kuwepo tena (talaka) na tatizo kubwa ni kwamba wengi
hukaa bila kuchukua hatua zinazostahili (serious) wakati tatizo au
mgogoro unapojitokeza ili kumaliza tatizo
Kutoshughulikia vizuri tatizo lolote kwenye ndoa hupelekea
Chuki,
Uchungu,
Kinyongo,
Kuumia hisia na
huweza kusababisha mwanandoa mmoja kujiondoa katika muungano wa kindoa uliopo
(kuanza kuishi kivyake katika kufikiria na kutenda).
Zifuatazo ni dalili mbaya sana ambazo zinaonesha ndoa inayoelekea kwenye kifo
KUFIKIRIA MAISHA KIVYAKO BILA MKE AU MUME KUMUHUSISHAUkiona
unaanza kufikiria uzuri wa maisha utakavyokuwa bila mwenzi wako kwa
maana kwamba kuwa na yeye unaona asilimia mia moja anakulostisha, au
hana maana kabisa ni dalili kwamba hiyo ndoa inaelekea kwenye kifo cha
ghafla.
Na kama unasongwa sana na mawazo kutaka kuishi mwenye au na
mtu mwingine zaidi ya huyo uliye naye na kujiona utakuwa na amani zaidi
basi unaelekea kubaya kwani inaonesha umeshapoteza nafasi yake ndani ya
moyo wako na kitu cha msingi waone washauri wa mambo ya ndoa ili waweze
kukusaidia.
MAMBO MABAYA NI MENGI KULIKO MAMBO MAZURI KWENYE NDOA YAKO
Kama mnajikuta ndoa yenu ina mambo mabaya mengi zaidi kama vile
kutokuelewana, k
ila mtu ana hasira,
mnapishana lugha kila mara,
hakuna kucheka wala kufurahishana na
mambo mazuri kama kucheka pamoja,
kufurahi pamoja,
kujisikia bila mwenzako siku haiendi
basi hiyo ni dalili kwamba hiyo ndoa inahitaji msaada na bila kuifanyia ukarabati basi itasombwa na mafuriko na hatimaye kufa.
UNAJISIKIA VIGUMU SANA KUWASILIANA NA MKE AU MUME WAKOJe, unajisikia kupatwa na hofu au mashaka kuongea na mke au mume wako kuhusu matatizo ya ndoa yako au maisha yenu kwa ujumla?
Mawasiliano ndiyo njia pekee ya kuondoa stress za ndoa na maisha kwa ujumla na hatimaye kujenga ndoa yenye afya kwa wanandoa.
Kama
mkiwa pamoja mnakuwa kimya bila kuongea chochote na hakuna dalili ya
kutaka kuongea na mwenzako basi kuna tatizo kubwa sana, hasa kama ni
tofauti sana na kawaida yenu hasa jinsi ilivyokuwa katika siku za kwanza
wakati mnachumbiana.
Kama hujisikii vizuri kuwasiliana na mwanandoa
mwenzio basi hiyo ni dalili kwamba tayari umekosa imani kwake na ndoa
huwa inakuwa katika wakati mgumu kukiwa kauna kuaminiana (trust)Pia
kama wewe ni mtu wa mwisho kujua kitu chochote muhimu au kuzuri kuhusu
yeye, basi hapo kuna tatizo kwani ni kawaida wanandoa kuelezana vitu
vizuri vinavyotokea kwa mmoja wao.
KILA MMOJA KUKATAA KUHUSIKA NA MATATIZO AU MIGOGORO YA NDOA INAPOJITOKEZAKama
kila mmoja anajilinda na kutothamini hisia za mwenzake hasa linapotokea
tatizo na kuanza kumrushia mwenzake lawana kwamba ndiye muhusika na
wote mnakuwa na msimamo huohuo, fahamu kwamba hapo ndoa inapitiliza hata
tiba za uangalifu zinazopatikana ICU.
Ikiwa migogoro au matatizo
yanapojitokeza kuna kuwa na kushindana kwa kila mmoja kukwepa kuhusika
na badala ya kupata suluhisho mnajikuta mgogoro unazidi kuongezeka basi
hiyo ni dalili kwamba sasa mmeanza kubusu kifo cha ndoa.
KUJIKUTA NI WEWE PEKE YAKO TU UNAHUSIKA KATIKA KUTATUA MIGOGORO AU MATATIZO YA NDOA.Je,
umekata tamaa, au kujisikia vibaya kuongea masuala ya matatizo ya ndoa
yako kwa sababu mwenzako anakurudisha nyumba, au imefika mahali na wewe
umeamua kunyamaza na kuachana kabisa na kujishughulisha na tatizo lolote
katika ndoa na matokeo yake hakuna hata mmoja anajali tena
kushungulikia matatizo ya ndoa?
Kama mpo
kwenye matatizo na kila mmoja amenyamaza kimya katika kuhakikisha
mnamaliza tatizo lililopo basi hii ndoa ipo ICU na kama mtabaki kimya
bila kila mmoja wenu kuhusika ili kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari
basi ni kama bomu lililotegwa ardhini na siku mtu akikanyaga hakuna
kitakachosalia.
TENDO LA NDOAKama
mmoja wenu sasa hana hamu kabisa na tendo la ndoa, au wote kwa pamoja
hamna hamu kabisa ya tendo la ndoa hiyo ni dalili kwamba somethings is
wrong.
Kukosa faragha ya pamoja (intimacy and
affection) itawafikisha mahali ambapo ndoa inaweza kufa au kuwa na ndoa
isiyokidhi haja au kukosa kuridhishana inavyotakiwa.
Je mnaishi tu kwa sababu ya watoto ndo wamewafanya msiachane?
Kama
ni ndiyo basi mnahitaji kupata msaada wa washauri wa mambo ya ndoa
kwani hakuna tatizo lolote kwenye ndoa ambalo halina jibu.
Kama
hakuna hamu ya mapenzi kwa mmoja wenu au wote maana yake hisia zenu
zipo mbali sana na hiyo ni dalili kwamba kila mmoja anaenda njia yake.
KUBISHANA AU KUGOMBANA KWA KITU KILEKILE KILA MARAKama kubishana, kupishana, kugombana, kuanzisha zogo kila mara kunatokana na issue
ileile moja bila kupata suluhisho basi hiyo ndoa imesimama haikui wala
kuelekea kwenye uimara zaidi bali inatelemka kwenda kwenye shimo.
Kama hakuna kitu kipya kinatokea ili kupata ufumbuzi wa hiyo hali basi tafuta mshauri wa mambo ya ndoa ili awasaidie.
HITIMISHO
Hakuna
tatizo la ndoa ambalo halina jibu hapa duniani kuna washauri wa mambo
ya mahusiano na ndoa, wazazi ambao hupenda mafanikio ya watoto wao, kuna
wachungaji ambao wana hekima na busara walizopewa na Mungu kwa ajili ya
kuwashauri hivyo hata kama kuna tatizo kubwa namna gani jibu lipo na
tiba ipo.
Anza kwa kuzungumza na mwanandoa
mwenzako then ikishindikana nenda kwa watu mnaona wanaweza kuwasaidia,
usiwe mbishi wala mbabe ndoa ni kuchukuliana na kuelewana.
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!