Buhari: Nigeria imekuwa maskini ghafla
Kiongozi wa Nigeria Muhammadu
Buhari amelalamika kwamba taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika limekuwa maskini ghafla.
Amesema hayo siku moja tu baada ya
Afrika Kusini kutwaa tena nafasi ya taifa lenye uchumi mkubwa barani Afrika.
Nigeria ilikuwa imeshikilia nafasi hiyo kwa miaka miwili baada ya kutathmini upya uchumi wake.
Afrika Kusini iliipita Nigeria baada ya kutumiwa kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha dhidi ya dola ya Marekani.
Sarafu ya rand ya Afrika Kusini imeimarika pakubwa ilhali naira ya Nigeria imeshuka sana.
Kwa sasa, thamani ya uchumi wa Afrika Kusini ni $301bn (£232bn) nao uchumi wa Nigeria $296bn.
Mataifa yote mawili hata hivyo si thabiti kiuchumi.
Akiongea mjini Abuja, Bw
Buhari
alisema: "Umekuwa mwaka mgumu sana kwa Nigeria. Kabla yetu kuingia
madarakani, mafuta yaliuzwa $100 (£77) kwa pipa. Bei hii ilishuka hadi
$37, na sasa ni kati ya $40 na $45 kwa pipa."
"Ghafla, tumekuwa
taifa maskini, lakini kujitolea kwetu kuhakikisha uwazi na uwajibikaji
kunazuia wananchi kuhisi kwamba kuna upungufu mkubwa katika uchumi."
Bw
Buhari alichukua mamlaka mwaka jana baada ya kushinda uchaguzi wa urais.
Aliahidi kukabiliana na ufisadi na kuinua uchumi wa Nigeria.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!