BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk James
Mataragio.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya shirika hilo na wadau mbalimbali wa
masuala ya mafuta na gesi, zimeeleza kuwa kusimamishwa kazi kunatokana
na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) ya mwaka jana iliyoeleza
kuwa, TPDC ilikiuka taratibu za manunuzi ya umma kwa kuipa upendeleo
kampuni ya Marekani kutafiti mafuta na gesi katika maeneo ya kaskazini
na magharibi mwa Ziwa Tanganyika, Songosongo, Mandawa na Eyasi.
“Shirika kwa sasa si salama, kwani mkurugenzi amepewa barua kutoka kwa
mwenyekiti wa bodi kusimamishwa kazi kuanzia jana (Jumatano) kutokana na
ripoti ya ukaguzi,” alisema mmoja wa watoa taarifa.
Hata hivyo, mpaka jana jioni hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, alisema anafahamu suala la kusimamishwa
kazi kwa Dk Mataragio, lakini akaongeza kuwa, maelezo zaidi kuhusu
maamuzi hayo anayo Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Profesa Sufian
Bukurura.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alipotafutwa kwa simu kutoa taarifa rasmi za
kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, hakupatikana kwani mara zote
simu yake ilisema inatumika.
Usisahau Kulike Ku-koment na Kushea.....
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!