Dunia imekwisha! Ndiyo sentensi pekee inayoweza kukutoka baada ya kusikia kisa cha
binti huyu aliyejitambulisha kwa jina la Malkia Said a.k.a Malkies, mwenye umri wa
miaka
19, mkazi wa Magomeni jijini Dar ambaye amekiri kujihusisha na vitendo
haramu vya usagaji akieleza alivyotembea na wanawake wenzake wasiopungua
40 wakiwemo
wake za
watu zaidi ya 20 hadi kufikia hatua ya kufumaniwa na kunyolewa nywele.
KABLA YA KUFUNGUKAKabla ya kufunguka yote hayo, awali
habari zake zilivuma kutoka pande mbalimbali jijini Dar na kwenye
mitandao ya kijamii ikidaiwa kwamba, mrembo huyo ni hatari kwa
wake za
watu hivyo wenye ndoa zao wakae chonjo.
Baada ya kuvuma kwa jina hilo la Malkies na sifa zake tajwa hapo juu huku ikidaiwa
kuwa alifumaniwa na mke wa mtu ndipo gazeti hili likajipa kibarua cha kumtafuta
binti huyo ili kujua mbivu na mbichi za msichana huyo.
HUYU HAPA MALKIESAkizungumza na waandishi wetu ndani ya
ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar, mapema wiki hii, huku akiwa
macho makavu, Malkies alisema
kuwa, alianza mchezo huo tangu akiwa mdogo kutokana na hisia za
mapenzi zilizokuwa zikimsukuma kwa kasi kujihusisha na kitendo hicho haramu.
“Nilipokuwa mdogo, kuna binamu yangu mara kwa mara alikuwa akinivizia
akitaka kunibaka lakini nikawa ninamchenga, sasa baba yangu alipofariki
dunia nikiwa darasa la nne ndipo nikapelekwa shule moja ya boarding
iliyopo jijini Mwanza.
“Muda mwingi nilikuwa na watoto wa kike wenzangu huku msukumo wa kufanya nao
mapenzi ukinitesa.
“Kwa
kuwa yule binamu yangu alisababisha niwe na hisia kali za
mapenzi, nikawa navumilia. Mwisho, nilihamishiwa shule nyingine ya boarding ipo Kibaha (Pwani).
“Huko
kuna siku nikawa naumwa, rafiki yangu Mzanzibari akataka kunichumu
shavuni. Ndipo tukajikuta tumeingia kwenye mchezo huo rasmi. Nakumbuka
hiyo ilikuwa mwaka 2010,” alisimulia Malkies huku akilengwalengwa na
machozi.
ASHTUKIWA SHULENIAlisema, baada ya hapo ilifikia hatua
uongozi wa shule ukajua na kuwaambia ndugu zake, akiwemo mama yake
lakini walipuuza kwa kuhisi anasingiziwa.
Alisema kadiri siku
zilivyosonga ndivyo alivyokubuhu na kupata uraibu uliomfanya kutotamani
kuuacha mchezo huo ambao aliamini ndiyo furaha pekee kwake kwani baada
ya muda, mama yake naye alifariki dunia.
AJARIBU
KUWA NA WANAUME
Alidai
kuwa, kutokana na maneno ya kila kukicha
watu wakimkemea juu ya ishu hiyo, Malkies aliona bora ajaribu
kuwa
na mwanaume labda anaweza kuacha, lakini kila mwanaume aliyekuwa naye
ambao wanaweza kufikia ishirini, hakuwa akihisi msisimko kama anapokuwa
na wanawake wenzake.
“Pia mjomba wangu alikuwa akinikuta na wanaume, ananipiga kwa sababu
aliona umri wangu hauruhusu na hakujua kwa nini nafanya hivyo maana
nilishindwa kumwambia,” alisema Malkies mwenye umri mdogo lakini
aliyepitia mambo mengi ya kikubwa.
AFUMANIWAAkiendelea kusimulia, Malkies alisema, kwa
kuwa anajitambua na anajua nini anachokifanya, alidhani ni vyema kutoka na
watu waliomzidi umri kuliko kuwapotosha vijana wa rika lake, ndipo akampata mke wa mtu.
Alisema kabla ya hapo alishakuwa na
wake wengine wa
watu lakini huyo wa Magomeni hali ilikuwa mbaya kiasi cha kutwangwa talaka na mumewe.
“Nimeshakuwa na
wake za
watu zaidi ya ishirini, wengi wamenizidi umri pia
wake za
watu
wananitaka wenyewe, huyo mmoja alikuwa anaishi Magomeni na mumewe akawa
ananishumbua kwa kipindi kirefu wakati mimi nilikuwa na mtu wangu.
“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoachana na huyo mtu wangu (mwanamke mwenzake), niliamua
kuwa na huyo mwanamke.
“Yeye ana umri wa
miaka 30, alinidanganya anaishi na baba yake, akanipeleka hadi kwake. Baadaye aliniweka wazi
kuwa anakaa na mumewe na majirani wakamfikishia habari mume
wake kuwa huwa nakwenda pale akiwa hayupo.
“Kulitokea ugomvi mkubwa kati ya yule mwanamke na mumewe, yule mwanamke akadai talaka na akapewa kwa sababu yangu.
“Niliendelea naye hata baada ya mumewe kumuacha, tukawa tunaishi wote
Ubungo kwa dada yake na mimi nikiwa na mtu najiachia kimahaba siwezi
kuficha.
“Wiki mbili baadaye, yule dada’ke alichukia, akaita ndugu zake na yule mume, wakaja kunifumania, wakanipiga na kuninyoa nywele.
“Tuliendelea kidogo lakini sasa tumeachana kabisa,” aliongeza
binti huyo ambaye pia aliwahi kushiriki kwenye filamu na muziki japokuwa hakuwika.
STAA ANAYEMZIMIKIAAkiendelea kueleza kwa kujiamini,
Malkies alisema, wanawake wengi ambao alikuwa akiwazimia ni Wazungu na
chotara, lakini mbali na hao alikuwa akiumiza kichwa na staa wa filamu
za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kumtunza Sh. milioni moja
kwenye shoo huko Arusha.
“Hakuna msanii anayenivutia zaidi ya Wema na
siku ile nilipomtunza ni kwa sababu tu alikuwa amelewa na mimi
nililewa, lakini tungekuwa sawa ningemueleza jinsi ninavyomkubali,”
alisema.
LENGO LA KUJITANGAZAAlimalizia
kuwa, suala hilo siyo jambo la kufumbia macho kwa sababu linafanywa na wanawake wengi wakiwemo mastaa na
wake za
watu
hivyo ameamua kuanzisha shirika la kuwasaidia wengine ambao bado
hawajajiingiza na waliojiingiza kwenye vitendo hivyo ili waache kwa
lengo la kuokoa kizazi hiki na kijacho.
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!