Bell 9 Atinga Kambi ya WCB, Afanya Mazoezi na Diamond:;

Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa
muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya
label hiyo.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’
ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.
Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na Diamond
wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza.
Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona
huweza WCB ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko.
Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!