Baraka Da Prince Kayatoa ya Moyoni Waliosema Kashindwa Kuongea Kiingereza:;

Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Baraka Da
Prince kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 aliingia kwenye headlines
baada ya mpenzi wake Najma kuonekana kuwa kama mkalimani wake kwenye
interview ya MTV Base.
Baraka Da Prince na kuyaongea ya moyoni:
Unajua watanzania asilimia kubwa wanakuwa wanakurupuka sana mimi sijaona
kwanza kitu cha ajabu cha mimi kutumia lugha ya Kiswahili, mimi
nimeenda MTV Base nimeulizwa Je unataka kutumia lugha gani ili uwe huru
nikawajibu ninaweza nikatumia lugha ya Kiingereza lakini sitokuwa huru’–
‘Sasa wabongo walifurahi wengine wakasema nimeshindwa kuongea kingereza
kwangu mimi nimeitangaza lugha yangu ya kiswahili halafu Najma hakuwa
mkalimani wangu mimi bali alikuwa anawambia yule mtangazaji kile
ninachokizungumza mimi’- Baraka Da Prince
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!