Asasi Zinazotetea Ushoga Zachunguzwa:;

SERIKALI inazichunguza asasi za kiraia zenye mwelekeo za kuunga mkono
ushoga na ndoa za jinsia moja na zitakazobainika zitachukuliwa hatua
kali.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison
Mwakyembe wakati akizungumza na uongozi wa asasi ya Mtandao wa Jinsia
Nchini (TGNP) ofisini kwake Dar es Salaam.
Alizitaka asasi hizo kutokubali shinikizo kutoka kwa nchi zinazowapa
misaada zenye nguvu kiuchumi za kutaka nchi zinazoendelea na asasi hizo
zikubali ushoga na ndoa hizo za jinsia moja kama sehemu ya haki za
binadamu ili kuendelea kupata misaada kutoka kwao.
“Nchi hizo zimekuwa zikitoa shinikizo kwa nchi zetu na hasa asasi nyingi
zikizitaka zikubali ushoga na ndoa za jinsia moja, nazichunguza asasi
zote za kiraia zenye mwelekeo huo na tukibaini mapungufu hayo
tutazichukulia hatua kali za kisheria, uchafu na upuuzi huo wa wazungu,
ubaki hukohuko kwao,” alisisitiza.
Waziri Mwakyembe alionya kuwa nchi ikilegeza kamba katika suala hili,
“tutashinikizwa baadaye kufunga ndoa na wanyama wa kufungwa kwamba nayo
ni sehemu ya haki za binadamu”.
Dk Mwakyembe amezitaka asasi hizo zisiyumbishwe na misaada kutoka nje
yenye mwelekeo huo wa kukinzana na mila, desturi, utamaduni, imani za
Watanzania, sheria na Katiba ya nchi.
Alisema serikali inaunga mkono juhudi za asasi mbalimbali za kiraia kama
vile TGNP za kuelimisha jamii na kutetea haki za watoto, wazee,
wanawake, walemavu na makundi mengine maalumu yanayostahili fursa na
haki sawa katika jamii, lakini haitazivumilia asasi ambazo zinaenda
kinyume na maadili na kukiuka sheria na taratibu ambazo nchi imejiwekea.
“Serikali inaunga mkono kazi zinazofanywa na asasi za kiraia nchini,
lakini niweke wazi kuwa hatutazivumilia asasi za kiraia zinazoyumbishwa
na misaada kutoka nje na kujihusisha na vitendo ambavyo vinakiuka
maadili, taratibu na sheria za nchi ambazo zipo kwa mujibu wa sheria,”
alisema.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amon Mpanju, alisisitiza umuhimu
wa asasi za kiraia kuisaidia serikali kwa kupeleka kwenye jamii ujumbe
sahihi wenye mafundisho, badala ya kusubiri kukosoa tu na kuzitaka asasi
za kiraia kuacha kuunga mkono hoja za ushoga kwa kishawishi cha fedha
wanazopewa kutoka kwa wafadhili wao.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!