AFYA YA MWANAMKE NA HEDHI SALAMA:;
KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA KIKE NA SULUHISHO LAKE JIKONI KWAKO
Kwanza napenda kuwashukuru wote mnaofatilia masomo yangu, kama unavitiwa
basi share na wenzako kisha kama una chochote basi usisite tuandikie
kwa namba 0758157247 whatsapp/text.
Napenda niseme tu kwamba moja ya sababu kubwa iliyonigusa kuandika elimu
hii juu ya kuvurugika kwa homoni za kike ambazo ni
estrogen,progesterone, Follicle Stimulating Homon,Luteinazing Hormon na
Testotestorone. Kwani tatizo hili limekuwa ni tatizo ambalo kila
mwanamke analo na wengi wao wametumia kila mbinu ya kuondoa tatizo na
wameshindwa. Basi leo utajifunza jinsi gani unavyohangaika kuangamiza
sisimizi kwa kutumia bunduki na ni uharibifu wa miundo mbinu katika
uhalisia kwani hukuzaliwa na matatizo hayo, ulikuwa mwenye afya tele na
unayefurahia hedhi yako bila tatizo.
MAMBO YANAYO ASHIRIA UNA TATIZO KATIKA HOMONI ZAKO ZA KIKE
1. Kuwa na hedhi ya muda mrefu Zaidi ya siku 7 unatumia Zaidi ya pedi 2
2. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana
3. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu,kuharisha
4. Kuwa na hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
5. Kuwa na hedhi ambayo haina mpangilio, Unaweza kuingia mara tatu kwa
mwez mmoja, mara mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi 6 hadi
mwaka.
6. Kuwa na ndevu sehemu za usoni,kifuani nyingi kupita kiasi
7. Kuwa na kitambi cha tumbo la chini (Abdominal obesity)
8. Kukosa mtoto kwa muda mrefu
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa lenye kuambatana na maumivu makali
10. Mwili kuwa unauma sana hasa misuli bila sababu ya msingi, kuumwa sana na kichwa bila sababu ya msingi.
Nimekuwa nikitafutwa na wakina mama wengi sana na wamekuwa wakinisimulia
jinsi gani wamesumbuka na kutatua tatizo hilo. Kusema kweli huwa ni
watu ambao napenda kuwaweka katika makundi yafuatayo halafu wewe
utajitambua upo kundi lipi.
1. Kundi la kwanza ni wale ambao ndio tatizo nimeanza kuwaandama na
hivyo wanajaribu kutafuta njia nyepesi za kuondoa tatizo kabla
hawajafikia zile njia ngumu za hospitali za kuliondoa tatizo. Wanawake
wengi huwa ni woga sana wa kuguza uzazi wao hasa pale inapotokea
hajaolewa na hajapata mtoto hivyo ikitokea ana tatizo kama hilo wengi
huwa wanakuwa makini kutojishirikisha na njia hatarishi. Afya yako ni
hazina yako wewe ndiye mwenye mamlaka wa kuruhusu tiba flani itekelezeke
au hapana.
2. Kundi la pili ni wale watu ambao wametumia kila mbinu za kutatua
matatizo kwa kuanzia ngazi za juu lakini hawapata suluhisho. Sasa
anaanza kutafuta suluhisho kwa upande wa pili ili aone kama na huko pia
atafanikisha kuifikisha afya yake mahali stahiki. Hawa huwa wamesumbuka
kwa wataalamu mbalimbali lakini hawajakata tamaa.
3. Kundi la tatu ni wale watu waliotumia njia zote bila mafanikio na
hadi wametamkiwa na washauri wao hapo hutaweza kufikia malengo, shusha
pumzi yako ipokee hali yako maisha yaendelee. Hawa ni watu ambao
wanaishi katika msongo wa mawazo mkubwa sana ambao sitamani hata
kuelezea mpendwa. Siri kubwa ambayo nakumegea ni kwamba Hukuzaliwa na
matatizo hayo Ulikuwa mwenye afya tele na mwenye kufurahia hedhi yako.
Mwanamke huwezi kuwa na Amani kama hedhi yako ina kasoro,kwani hio ndio
nyota njema katika maisha yako kiafya ya kila siku ni jukumu letu
kuhakikisha inarudi katika misingi ya mwanzo na ufurahie hedhi yako.
Nina Imani kwamba umetumia njia nyingi sana, na kama ndio umehitimisha
na umekata tamaa basi napenda nikushauri kwamba ili uweze kunielewa
vizuri katika haya machache hakikisha Unatupilia mbali yote ambayo
ulishauliwa kuyafanya na hayajakupa matunda yote unayojua kichwani
mwako inawezekana kabisa hayana faida yoyote na inaweza kuwa ni chanzo
moja wapo cha kukuzuia wewe kurudiaa afya yako njema. Hebu kuwa kama
hujui kitu ili elimu hii ianze marekebisho ya afya yako.
Hukuzaliwa na kitambi,hukuzaliwa na ndevu,hukuzaliwa na maumivu makali
kiasi hicho ya hedhi na hukuzaliwa ukiwa na mtu mwenye mateso kuhusu
afya yako ya hedhi sasa hizi ndizo njia rahisi ya kuondoa tatizo kwani
inawezekana wewe ndiye kisababishi kikubwa cha lishe mbovu inayokuuguza
kila siku.
UGONJWA WA POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
Mwanamke huwa ana viwanda viwili vya kuzalisha mayai kila mwezi yaani
kwa lugha nyingine ni Ovari ya kushoto na Ovari ya kulia. Ndani ya ovary
ya mwanamke kuna mayai ambayo hayajakomaa kwa lugha ya kilatini huitwa
Follice cells ,hizi ndizo hukomazwa kila mwezi na kutupatia yai ambalo
linatakiwa lipatiwe urutibishaji endapo itakutana na mbegu ya kiume.
Sasa inapotokea hizo follicle cells zimekomaa vizuri kwenye ovary na
zinatakiwa zipasuke zitoe mayai bahati mbaya kabisa Kitendo hicho
kinashindikana hivyo hizo follicles ambazo zimeshindwa kupasuka na kutoa
yai zinabaki na umbo kama Zabibu zilizo kwenye kikonyo chake mwonekano
wake kwa kitaalamu zinafananishwa na kitu kiitwacho Cyst kwa sababu zipo
nyingi tunatumia neno la kitalamu Polycystic. Na hii hali huambatana na
dalili nyingi ambazo zinauvuruga mwili wako kwa sababu ya ovary zako
kutengeneza cyst nyingi Polycystic kwa pamoja dalili hizo tunaziita
Syndrome neno hili humaanisha Mkusanyiko wa dalili nyingi.
Kwa hio basi kitendo cha ovary zako kushindwa kutoa mayai kama kawaida
na hatimaye kutengeneza polycysts nyingi kwenye ovary inakupelekea
unapata ugonjwa uitwao Polycystic Ovarian syndrome Ovary yako inaonekana
kama zabibu ambazo hazijatolewa kwenye kikonyo chake zilivyokusanyika.
Neno cyst ni kitu chenye uwazi kwa ndani na kimezungushiwa ukuta
mwembamba na laini (Membrane). Na mle ndani kunaweza kukaa
damu,usaha,maji nk. Lakini kwa upande wa mwanamke hizo follicles nyingi
ambazo zimekomaa na zimeshindwa kutoa mayai zinafanishwa na Cysts
lakini jina halisi ilitakiwa kuwa POLYFOLLICULAR SYNDROME, kwa sababu
follicles nyingi katika ovary zimeshindwa kutoa mayai na zinaonesha
mwonekano kama Cysts
NINI KINAPELEKEA UNAPATA UGONJWA HUU WA POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME-PCOS
1. Kuongezeka kwa homoni za kiume zinajulikana kama Androgens ambazo ni
Testosterone. Kwa kawaida mwanamke huwa ana kiwango kidogo sana cha
homoni hii ya kiume Testosterone Homoni inayomfanya mwanaume aonekane
mwanaume kuongezeka kwa homon hii inampelekea mwanamke kuonesha dalili
za kuongezeka kwa dalili za kiume kwa mwanamke kama kuota ndevu
kidevuni,chunusi sugu na pia kuongezeka uzito kupita kiasi na kitambi
pia.
Homoni hizi zinatengenezwa na ovary za mwanamke na tezi ya adrenali
baada ya kupata msukumo kutoka kwenye homoni iitwayo insulin. Kwa hio
basi watu wenye kiwango kikubwa cha insulin wapo hatalini kupata ugonjwa
huu wa PCOS na ndio maana watu wengi wenye PCOS ukubwani huwa ni ishara
moja wapo unaelekea kupata ugonjwa wa kisukari maana yake upo hatua za
mwanzo yaani Pre diabetic ambapo hatua ambayo kwa nchi zinazo endelea
tunaweza kukubaini kwa kutumia dalili zinazo unazo na sio kwa kipimo
maana kiwango cha sukari huwa kipo sawia kabisa lakini unakuta insulin
ipo juu changamoto inakuja hatuna vifaa vya kupita kiwango cha insulin
kwenye damu. Hivyo basi njia rahisi ya kukubaini haraka kama upo hatua
za mwanzo ni kuangalia dalili gani ulizo nazo.
Mbali na nywele sehemu za kidevu kuonekana,chunusi sugu, uso wenye
mafuta mengi sana kupita kiasi,shingo kuwa nyeusi sana na sehemu zingine
kama kwapa na kwenye mikunjo sehemu za siri kwa kitaalamu inaitwa
Acanthosis Nigricans pia hata kupata viotea shingoni yaani Skin Tags
pia ni dalili kuwa kiwango cha insulin kipo juu na upo Pre diabetic na
endapo ukiamua kurudisha afya yako upya unaweza kabisa. Zote hizo ni
dalili moja wako kwa wananwake wanaosumbuka na PCOS.
Hebu sasa tujiulize swali moja kubwa! Kumbe homoni ya Testosterone
inapokuwa katika kiwango cha juu kupita kiwango maalumu kwa wanawake
inampelekea mtu kupata PCOS! Na hii homoni kuongezeka kwake ni pale
insulin inapo enda kuamuru Tezi ya Ovary na Adrenali kutoa homoni za
Kiume kwa wingi kupita kiasi.
Swali: Kama ndivyo hivyo swali la kujiuliza sasa kwa nini wagonjwa wenye PCOS wapo hatarini kupata kisukari
JIBU: Wagonjwa wenye PCOS wapo hatarini kupata ugonjwa wa kisukari maana
wote huwa wana kiwango kikubwa cha insulin kupita kiasi kwenye damu
kama ishara ya Insulin resistance kwa lugha nyingine Insulin
Tolerance yaani seli za miili yao huwa haziwezi kubaini uwepo wa
insulin kwenye damu na hivyo insulin huwa haifanyi kazi yake ipasavyo.
Na hii hali ya seli za mwili kutoweza kubaini uwepo wa insulin kwenye
damu inasababisha sukari katika damu kutofanyiwa kazi na hatimaye sukari
inaanza kupanda na kukupelekea kupata kisukari Hali ya sukari kwenye
damu kuwa katika kiwango cha juu muda wote kwenye damu kiwango hiki
kingi cha insulin ndicho kimekuwa kichochezi kikubwa kwa wana wake wengi
kuugua ugonjwa huu!
Swali: Nini kinasababisha insulin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ipasavyo
Neno Insulin resistance limekuwa likitafsiriwa tofauti sana na watu
wengi hasa washauri wa afya. Lakini tafsiri mbaya kabisa ambayo hata
wewe unayo hapo ni kwamba insulin inaposhindwa kufanya kazi maana yake
mafuta mabaya yameziba kwenye kipikea insulin Insulin receptor na
hatimaye insulin haiwezi tena kufanya kazi. Huu ni Uongo kabisa tena
ulio wazi!
Ili uweze kunielewa vizuri nakupa tafakari nzuri hapa kama mbili ili uje unielewe vizuri.
1. Nazani kila mtu anajua jiji la Dar es salaam lilivyo na joto kali
kupita hali ya hewa ya mikoa mingine yote. Mtu ambaye ni mkazi wa mwanza
ukimleta jijini lazima atasumbuka sana kuzoea joto hili. Na ndio maana
sasa baada ya kukaa miezi kama 6 anakuta amezoea mazingira haya anaona
kama hakuna utofauti kabisa. Maana yake mwili wako umezoea mazingira
You have Tolerated the hot climatic condition neno kuzoea naweza kusema
ni sawa na kulipa maana ya Tolerance au Resistance
2. Pia chukulia mfano mlevi wa pombe kali kama Dompo mwanzo alikuwa
nakunywa chupa mbili na analewa sana hadi kuendesha gari hawezi. Lakini
kadri muda unavyo enda atajikuta anapiga pombe hizo chupa mbili hata
halewi chochote kabisa. Maana yake zile chupa mbili zimemzoea haziwezi
tena kufanya kazi yake Kumlewesha kama zamani. Hivyo kwa lugha
nyingine hizo chupa mbili za dompo mwili wako ume Tolerate au Umepata
Resistance dozi inatakiwa iongozwe ili ulewe Zaidi.
3. Mfano wa mwili ni pale unapo ambiwa na washauri wa afya usitumie
antibiotic hovyo hovyo maana wale wadudu watazoea hizo dawa na hatimaye
isiwe rahisi kuwatibu kwa dawa hizo ndio maana tunaambiwa tupime kwanza
kabla ya kunywa dawa ili kupunguza matumizi ya dawa hovyo na kusababisha
dawa zingine kutokuwa na uwezo wa kuangamiza vimelea.
Haya nahitimisha kwamba kitu kinacho sababisha Tolerance au Resistance
ni kile kile . mfano yule ambaye alisema dar kuna joto sasa joto lile
lile amelizoea. Aliyesema pombe mbili nalewa sasa pombe ileile haiwezi
kumlewesha, na dawa kutofanya kazi yake kisababishi ni matumizi ya
madawa hovyo.
Hivyo basi hata kongosho la binadamu linapomwaga maji ya insulin kwa
kutumia seli zake aina ya beta moja kwa moja kwenye damu. Kadri
linavyozidi kuongeza kiwango chake kingi katika damu ndivyo itafikia
hatua seli za mwili zinapata Insulin Tolerance yaani hio insulin
haiwezi tena kufanya kazi yake ipasavyo.Hivyo kisababishi cha insulin
resistance au Tolerance ni insulin yenyewe.
Ulaji wa vyakula vya wanga kupindukia na vyakula vyenye sukari rahisi
vinasababisha kiwango cha insulin kumwagwa kwa wingi kupita kiasi na
hatimaye kupelekea insulin kuwa katika kiwango cha juu muda wote na
mwishowe insulin inakuwa haiwezi tena kufanya kazi yake.
Kwa hio basi chanzo kikubwa cha insulin kuwa katika kiwango cha juu
kupita kiasi ni ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi. Na
tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na sukari vinaongoza
kupandisha kiwango cha insulin mwilini mwako,ikifuatiwa na vyakula vya
protini na vyakula vya mafuta vimeonesha havina madhara kabisa ya
kuongeza insulin katika damu baada ya kula. Ukitaka kuifanya insulin
ifanye kazi ni kupunguza vitu vinavyo ongeza kiwango cha insulin.
Hii ndio maana wagonjwa wengi wenye PCOS wanapewa dawa kama Metformin
dawa za kuongeza utendaji kazi wa insulin yaani inaondoa Insulin
resistance lakini hilo sio suluhisho la kudumu katika maisha yako na
suluhisho pekee ni kuhakikisha vitu vinavyopandisha insulin vinaepukwa
na utashangaa maajabu yake.
Hivyo basi napenda kusema kwamba jiko lako linaweza kuwa linakuuguza
kabisa na ni wakati sasa wa kusafisha jiko lako na vyakula ambavyo
uliambiwa ni adui yako hebu kuanzia leo view rafiki yako mpendwa,
vyakula kama Nafaka yaani mahindi,mtama,ulezi nk,viazi,Ngano aina yoyote
vinywaji vyote vyenye sukari, pombe aina zote ,Epuka tambi , hivi
ndivyo vinavyokuuguza hata kama unatumia dawa ndio maana hupati mwafaka.
Safisha jiko lako sasaa!
Kula vyakula kama samaki,karanga,ufuta,alizeti,korosho,almonds,Nyama
aina yoyote,mayai nk kwani ni vyakula sana kwako na tiba kwako ndani ya
muda mfupi sana.
2. Ugonjwa huu ni wakurithi kwa asilimia ndogo sana
Napenda tu kukuambia kuwa ugonjwa huu wa PCOS ni ugonjwa wa lishe ambayo
haizingatii kanuni na masharti ya tiba. Watu tukiongea lishe mbovu
anajua ni ile hali ya kula vyakula vya mafuta,kula sana,kunywa pombe na
kutofanya mazoezi! Najua unawaza hayo maana umepotokavyakutosha
umejaribu kuyaepuka hayo na bado unaendelea kuugua kila siku. Tizama
sana kwa kina vyakula ambavyo vinavuruga homoni za mwili wako na
hatimaye kukuletea ugonjwa huu. Na nimeeleza kwa kina namna gani vyakula
vya wanga vinavyo tuletea ugonjwa wa PCOS na suluhisho lake.
Hivyo bas unapotaka kusema huu ugonjwa ni wakurithi hakikisha umeondoa
visababishi vingine vyote vya ugonjwa huo kwa kitaalamu tunasema
Genetic factor should be the diagnosis of Exclusion huwa nasema kila
siku huwezi kuniambia kwenu kuna watu wenye ndevu na wewe basi umerithi
ndefu kutoka kwa bibi yako sio kweli! Maana yake mmerithishana mapishi
mabovu yasiyozingatia afya ya uzazi wako. Hivyo neno kurithi huwa
sipendi kulisikia linakukuficha kifikra katika maradhi na unashindwa
kulitafutia suluhisho ukiwa mwenye nguvu tele.
NINI MADHARA YA HOMONI HIZI KUVURUGIKA MWILINI KWA MWANAMKE
Sayansi ya homoni Endocrinology naifananisha na vitabu kumi ambavyo
nimevipanga kwa wima kwenye meza, ikitokea nimekisukuma kitabu kimoja
kikaangukia kitabu cha pili yake vitabu vyote kumi vitaanguka kwa
kufuata mlolongo ule ule. Hii namaanisha kwamba homoni moja ikitoka
katika misingi yake homoni zingine pia zinavurugika kwa kiwango kikubwa
sana na ndio maana watu wenye PCOS huwa wana dalili Zaidi ya moja kwani
ugonjwa huu unahusisha mvurugiko wa homoni nyingi sana. Kumbuka usihofu
sasa tiba ya ugonjwa huu ni lishe hata wewe unaweza kuanza leo
kuhakikisha unasawazisha homoni zako zote zirudi katika misingi.
Zifuatazo ni baadhi ya homoni ambazo huvurugika mwilini mwako na mwisho wake unapata PCOS.
1. Kiwango cha Estrogen huongezeka kupita kiasi.Hii inasababishwa na
insulin kuisisimua ovary kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na hii
inapelekea kiwango cha homoni hii kuwa juu kwenye damu. Madhara ya
homoni hii kuwa katika kiwango kikubwa katika mwili wako inaweza
kukupelekea ukuta wa kizazi kujengeka na kuwa mnene kupita kiasi
Endometrial hyperplasia na hatimaye unaweza kuwa hatarini kupata kansa
ya kizazi. Na hii ndio sababu kubwa ya kupata hedhi nzito kupita kiasi
yenye mabonge ya damu sana, kwa sababu kazi kubwa ya estrogen ni
kukufanya wewe uonekane mwanamke na ndio homoni ambayo inajenga ukuta
wa kizazi kila mwezi ili kama mimba ikitungwa mtoto aje ajishikize
kwenye ukuta imara. Lakini inapotokea kiwango chake ni kukubwa ukuta
mnene utajengwa kila mwezi na inapokuwa mimba haijatungwa ukuta
utabomolewa na kama ni mnene damu nyingi sana zitatoka hali hii tunaita
Polymenorrhea ukiona dalili hizo fika hospitali maana kuna hatari
kubwa ya kuishiwa damu.
2. Follicle Stimulating Hormon(FSH) inashuka kiwango
Hii ni homoni inayotolewa na upande wa mbele wa tezi ya Pituitary
kwenye ubongo baada ya kupata taarifa kutoka kwenye hypothalamus. Homoni
hii kazi yake kubwa huwa inakomaza mayai kwenye ovary za mwanamke. Sasa
kiwango hiki kinaonekana kuwa katika kiwango kidogo sana kwa mwanamke
mwenye PCOS kwa sababu kiwango kingi cha estrogen kwenye damu kinapeleka
taarifa kwenye ubongo kwamba homoni zipo zinajitosheleza (Negative
feedback inhibition) na hatimaye ubongo hautatoa taarifa yoyote ya
kutengenezwa kwa FSH. Na hii ndio sababu kubwa ya ugumba kwa wanawake
wenye PCOS kwani kama hii homoni ipo katika kiwango cha chini hakuna yai
lolote litakomazwa.
3. Homoni ya luteinizing (LH)
Homoni hii kwa wagonjwa wa PCOS huwa ipo pia katika kiwango cha kawaida
au chini na hivyo basi inakuwa haiwezi tena kufanya kazi yake ipasavyo.
Kazi kubwa ya Luteinizing homon ni kuishinikiza ovary itoe mayai kila
mwezi yale yaliyo komaa. Sasa kama haifanyi kazi yake hakuna kitakacho
timia katika zoezi zima la mayai kuja kwenye mirija ya uzazi kwa
kurutubishwa.
JINSI YA KUBAINI UGONJWA HUU KAMA UNAO AU HAPANA
Napenda tuweze kubaini ugonjwa huu kwako kwa kushirikiana na wewe
mpendwa,lakini wanasayansi hawakutaka kila mtu aje na tafsiri yake kwa
ugonjwa huu, tunatumia ROTTERDAM CRITERIA Huu ni mwongozo wa kuweza
kubaini mwanamke kama ana ugonjwa huu au hapana ambao una vitengo 3
vikubwa:
1. Dalili za magonjwa ya uzazi zote ambazo nimezitaja hapo juu. Kama unazo basi moja wapo kuzihusisha
2. Kipimo cha damu na kwenda kuangalia homoni za Estrogen,Testosterone,FSH,LH na Insulin
3. Kipimo cha mionzi ya tumbo (Abdominal Ultrasound)-Ikinonesha ovary ina cyst nyingi (Polyfollicular ovary)
Endapo ukiangukia katika vitengo kuanzia viwili au vitatu basi kuna
uwezekano mkubwa kuwa una ugonjwa wa POLYFOLLICULAR SYNDROME (PCOS).
MAKUNDI YA WATU WENYE POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
Hebu tizama makundi haya matatu maana kila mtu ambaye amekuwa
akinitafuta huwa anapenda sana nitoe ufafanuzi kuhusu ugonjwa huu, basi
leo nimeamua kukupa mchanganuo mwepesi kabisa uelewe kwa kina kama
ifuatavyo:
1. Kundi la kwanza ni mwanamke amepima amekutwa ovary zake zina
Poycysts ,hapati hedhi mara kwa mara yaani hedhi yake mbovu na ana
dalili za homoni za kiume (Nimezitaja juu)
2. Kundi la pili ni mwanamke mwenye ovary zenye Polycysts ana dalili
za homoni za kiume lakini Mzunguko wake upo vizuri ( Hawa wapo wengi
sana, ana ndevu, na ukipiga picha ya tumbo unakutana na ovary ina cysts)
na ukimwambia una tatizo anakwambia ndevu za urithi,weusi huu shingoni
ni wa urithi unaanza kutafuta dawa za kuondoa weusi za kupaka. Dawa ni
lishe tu unapona!
3. Kundi jingine ni mwanamke mwenye ovary zenye polycysts ,hana dalili
za homoni za kiume lakini mzunguko mbovu sana ( Huyu hana ndevu, hana
dalili zozote za kiume lakini hedhi yake inamtia mawazo kila mwezi)
4. Kundi la mwisho ni wale ovary zao zipo vizuri kabisa Ikipimwa
naambiwa hakuna cysts kabisa Lakini ana dalili za homoni za kiume na
mzunguko mbovu na yenye yenye kuambatana na maumivu makali sana kupita
kiasi. ( Hawa pia wengi sana kwani husema mimi sina PCOS kabisa nilipima
anashindwa kujua Rotterdam criteria imeweka makundi 4 baada ya
uchunguzi)
Napenda kukupongeza sana kufuatilia somo langu hili la afya ya mwanamke,hakikisha unashare na wenzako makal hii.
MTUMIE UJUMBE HUU RAFIKI YAKO YEYOTE AJIFUNZE NA AUNGANE NA SISI FACEBOOK, mkumbo healthcare products KUPATA ELIMU ZAIDI.
Kwa maoni, ushauri na Tiba basi usisite kutuandikia kwa whatsapp/text 0758157247.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!